Wananchi wa Kata ya Ilunde wakivuka Daraja la Mto Ipati baada ya kujaa Maji.
Na Walter Mguluchuma ,Mlele
Wananchi wa Kata yaIlunde katika Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi wamewashukuru wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Katavi kwa kuweza kuwarejeshea mawasiliano ya barabara kwa wakati iliyowaunganisha na makao makuu ya Wilaya yao ya Mlele ambayo iliyokuwa hapitiki kutonana na maji kupita juu ya daraja .
Meneja wa Tanroads Mkoa wa Katavi Mwandisi Martin
Mwakabende wakati alipokuwa kwenye eneo la daraja la mto Ipati
akiangalia namna ya kurudisha mawasiliano ya barabara ya kwenda Ilunde kutokana
na maji kupita juu ya daraja la mto huo
Wananchi wa Kata yaIlunde katika Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi wamewashukuru wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Katavi kwa kuweza kuwarejeshea mawasiliano ya barabara kwa wakati iliyowaunganisha na makao makuu ya Wilaya yao ya Mlele ambayo iliyokuwa hapitiki kutonana na maji kupita juu ya daraja .
Salome Mbaluku mkazi wa Kijiji cha
Ilunde amesema hari ilikuwa ni mbaya kwenye eneo hilo kwani
magari yalishindwa kupita kabisa kutokana na maji hayo hali ambayo ilifanya
baadhi ya watu wavuke kwa kubebwa migongoni na kutozwa kiasi cha kuanzia tshs
2000 hadi tshs 4000 kutegemeana na uzito wa mtu .
Maiko Kasagula mkazi wa Kijiji cha Ilunde amesema kuwa walikuwa
hawaamini kama mawasiliano hayo ya barabara yangeweza kurejeshwa kwa muda huo
mfupi kutokana na hari ilivyokuwa imeonyesha ni jinsi gani Serikali
inavyowajari wananchi wake mpaka wa pembezoni kama Ilunde .
Meneja wa Tanroads Mkoa wa Katavi Mwandisi Martin Mwabande
amesema kuwa taarifa ya kukatika kwa mawasiliano hayo walipata kutoka kwa
Diwani wa Kata ya Ilunde Martin Mgoroka na baada ya taarifa hizo
walifika kwenye eneo la tukio na kukuta mawasiliano ya barabara yakiwa
yamekatika kutokana na maji kupita juu ya daraja .
Amesema jitihada za haraka za kurejesha mawasiliano zilifanyika
kwa kupeleka haraka mndarasa aliyekuwa akifanya kazi kwenye barabara
ya Inyonga kwenda Maji Moto .
Mwakabende amesema kuwa pamoja na kufanyika kwa matengenezo hayo ya
dharula bado Tanroads wataendelea kuwepo kwenye eneo hilo la
daraja ili kuhakikisha wananchi hawakosi mawasiliano licha ya eneo hilo
kuwana maji mengi ya mvua yanayotokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwa sasa
.