Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akipanda Mti kwa pamoja na moja ya Mkazi wa kijiji cha Isinde katika shule ya Msingi Isinde Halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi. |
Na Paul Mathias-Katavi
Serikali ya katika mkoa wa Katavi imesema zoezi la upandaji miti ambalo limeanza toka Mwezi wa February Mwaka huu katika halmashauri za mkoa wa Katavi limeeweza kufanikiwa kwa kwa kiasi kikubwa ambapo hadi sasa Miti Milioni Sita imewezwa kupandwa katika maeneo Mbalimbali ya Taasisi za Umma na kwenye makazi ya Watu.
Wananchi na wadau mbalimbali wa mazingira wakishiriki zoezi la upandaji miti katika eneo la shule ya Msingi Isinde Halmashauri ya Nsimbo mkoa wa Katavi. |
Serikali ya katika mkoa wa Katavi imesema zoezi la upandaji miti ambalo limeanza toka Mwezi wa February Mwaka huu katika halmashauri za mkoa wa Katavi limeeweza kufanikiwa kwa kwa kiasi kikubwa ambapo hadi sasa Miti Milioni Sita imewezwa kupandwa katika maeneo Mbalimbali ya Taasisi za Umma na kwenye makazi ya Watu.
Mkuu
wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amebainisha hayo wakati akizungumnza na
wananchi wa Kijiji Cha Isinde Halmashauri ya Nsimbo mkoa wa Katavi ikiwa ni
Sehemu ya maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kufanya
shughuli za upandaji miti katika Shule ya Msingi Isinde.
amesema
kuwa tangu Shughuli Mbalimbali za upandaji wa miti zianze katika maeneo
mbalimbali ya mkoa wa Katavi hadi sasa kuna miti zaidi ya Milioni 6 imepandwa
katika mkoa wa Katavi ikiwa ni sehemu ya kutekeleza Maagizo ya viongozi wa juu
ya suala la utunzaji wa Mazingira
Mohamed Ramadhan mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Nsimbo akieleza utekelezaji wa zoezi la upandaji miti katika halmashauri ya Nsimbo |
‘’Mrindoko hapa anasema kwa takwimu ambazo tunazo mkoani na tumefatilia mkoa mzima kwa maana ya halmashauri zote Tano miti iliyopandwa ni zaidi ya million 6 na laki 9 lakini maelekezo ya Makamu wa Rais wetu na Rais kupitia wizara ya Mazingira nilazima kila halmashauri ipande miti Milioni 1 na laki Tano’’
Amesema
zoezi hilo la upandaji miti niendelevu na wiki ijayo litaanza kwa awamu ya pili
ikiwa ni sehemu ya kufikisha lengo la kupanda miti Milioni Saba na laki Tano
kwa mkoa wa Katavi.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Nsimbo Mohamed Ramadhani amsema kuwa halmashauri hiyo imekuwa
ikitekeleza agizo la Upandaji miti kwa kupanda miti katika sehemu mbalmbali za
halmashauri ya Nsimbo
‘’kwaajili
ya kupendezesha mji wetu kata hii ya Mtapenda nimiongoni mwa maeneo ambayo
yamepagwa ukitoka manispaa ya Mpanda mpaka kufika hapa hapa katikati pote
panaendelea kupimmwa na kupangwa barabara hii kutoka Nsimbo sekondari mpaka
hapa Isinde hadi makao makuu ya kata ni karibu kilomita Sita na barabara hii
inayopitia Mtapenda kwenda Manispaa tumepanda miti hivyo baada ya muda tutakuwa
tunapita kwenye kivuli kupitia miti tuliyoipanda’’ amsema Mohamed.
Kwa
upande wake Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna Lupembe ambae pia ni Makamu
mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya mazingira na Maji amesema kuwa kamati hiyo
imekuwa ikisistiza suala la uhifafadhi wa mazingira ikiwa nipamoja na Upandaji
wa Miti.
Mimi
kama makamu mwenyekiti wa kamati ya bunge ya Maji na Mazingira nimeona tuanze
hapa leo Isinde kwa kupanda miti ili kutunza Mazingira amesma Anna Lupembe
Mbunge wa jimbo la Nsimbo kwenye zoezi Hilo.
Zoezi la upandaji miti limefanyika katika shule ya Msingi Isinde na Shule ya Sekondari Anna Lupembe ambapo zaidi ya Miti 800 imeweza kupadwa kwenye zoezi hilo.