Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna Lupembe akiwahutubia wanamichezo waliojitokeza katika Bonanza la michezo kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Nsimbo Mapema leo. |
Wakazi wa Mkoa wa katavi
wameaswa kulichukulia suala la michezo kamasehemu ya ajira na Upendo na
mshikamano katika kwenye jamii.
Wakazi wa Mkoa wa katavi wameaswa kulichukulia suala la michezo kamasehemu ya ajira na Upendo na mshikamano katika kwenye jamii.
Akizungumnza katika Bonanza la Michezo lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Nsimbo Mbunge wa Jimbo Hilo Anna Lupembe amesema kuwa michezo imekuwa ni sehemu ya Ajira kwa vijana kwa kujipatia kipato kupitia michezo ya aina mbalimbali.
‘’sisi kama halmashauri yetu ya
Nsimbo tumeamua fedha za Jimbo tutumie kujenga viwanja vya hivi vya Mpira wa
Pete na Mpira kikapu ili kufanya maendeleo ya Michezo tukitambua kuwa michezo
ni Ajira, michezo ni furaha,michezo ni amani’’
Ameeleza kuwa bonanza hilo
limefanyika kwa kujumiusha Mikoa ya Dodoma,Rukwa,Tabora,Kigoma na Katavi kwa
lengo la kuutangaza mkoa wa Katavi hasa halmashauri ya Nsimbo katika sekta ya
Michezo .
Katika hatua nyingine amesema
kuwa tangu aanzishe Mashindano Mbalimbali kama Lupembe Cup kumekuwa na
mafanikio makubwa kwa baadhi ya vijana kupata fursa ya kujiunga na timu zenye
uwezo katika michezo na wengine kupata fursa ya kwenda nchi za nje kupitia
Mpira wa Kikapu.
Anna Lupembe anasema ‘’Ndugu
Mgeni Rasimi hapa tunakijana amepata fursa ya kupata nafasi ya Kwenda Marekani
kucheza Mpira wa kikapu haya ninamafakio makubwa sana katika sekta ya michezo
katika halmashauri ya nsimbo ndio maana nimekuwa muumini wa Suala la michezo
kwa vitendo ‘’
Michael Kadebe Rais wa shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania TBF akitoa neno kuhusu umuhimu wa Mpira wa Kikapu kwa vijana |
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa
katavi Mwanamvua Mrindoko ambae alikuwa Mgeni Rasimi katika Bonanza hilo la
michezo katika halmashauri ya Nsimbo amesema kuwa Mmbunge wa jimbo la Nsimbo la
Nsimbo Anna Lupembe ni mfano wa kuigwa katika sekta ya michezo katika mkoa wa
katavi
‘’Mbunge huyu amekuwa amfano wa
kuigwa katika sekta ya Michezo utasikia ametoa Mipira,ametoa majezi,ametoa
amagoli hiii inaonyesha nikwa namna gani wanansimbo mmepata Mbunge wa vitendo
hongereni sana’’
Mkuu huyo wa mkoa ametumia
fursa hiyo kuwaagiza wakurugenzi wa halmashauri kulipa kipaombele suala la
michezo kwa kuhakikisha mazingira na miundombinu ya michezo iunajengwa kwa
kujenga viwanja vya kisasa.
Mkuu wa mkoa wa Katavi mwanamvua mrindoko akizungumnza na wanamichezo kwenye bonanza la michezo lililofanyika viwanja vya shule ya sekondari Nsimbo |
Ametoa wito kwa wazazi
kuwaachia watoto wao kujifunza michezo hii kwakuwa bado inaonekana kuwa na
fursa kubwa katika mataifa mengine.
Katika bonanza hilo michezo mbambali ya Mpira wa Miguu kikapu na pete limefanyika kwa kuchezwa michezo kwa kushirikisha wanamichezo kutoka mikoa ya Dodoma,Kigoma,Rukwa,Tabora na Katavi.