Na Paul Mathias- Katavi.
Jamii ya Watanzania imeobwa kuungana na serikali katika Mapambano ya Wimbi la ushoga ulawiti na usagaji ambalo limeonekana kushamili kwenye baadhi ya Jamii za Kitanzania ili kulinda maadili na utu wa Mwafrika.
Jamii ya Watanzania imeobwa kuungana na serikali katika Mapambano ya Wimbi la ushoga ulawiti na usagaji ambalo limeonekana kushamili kwenye baadhi ya Jamii za Kitanzania ili kulinda maadili na utu wa Mwafrika.waumini wa dini ya kiislamu katika mkoa wa katavi wakiwa katika swala ya Eid el fitri katika viwanja vya shule ya msingi Kashato.
‘’Ikiwa
wanawake wataona wao kwa wao wanasagana na wanaume kuoana wao kwa wao kizazi
kitaongezeka vipi nilazima kilammoja wetu tukemee jambo hili kwa nguvu zetu
zote watu wawa fichue mashoga popote pale walipo ukimjua huyu ni shoga mwambie
mwenzako jamaa ni shoga,,amesema Shekhe Mashaka.
Amesema
kuwa wao kama viongozi wa Dini wanayasema hayo kwakuwa wanaoahtirika na vitendo
hivyo ni pamoja na watoto wadogo kufanyiwa vitendo vya ulawiti hivyo kila
mwanajamii lazima kuchukua tahadhari juu ya matendo hayo maovu.
Waumini wa Dini ya kiislamu katika mkoa wa Katavi wakiwa katika swala ya Eid el fitri iliyoswaliwa katika viwanja vya shule ya Msingi Kashato |
Aidha
katika hatua nyingine ameeleza kuwa ikiwa kutakuwa na Mpango maalumu wa kupima
ili kuwabaini Mashoga viongozi wa Dini ya kiislamu katika mkoa wa Katavi watakuwa
wa kwanza kupima ikiwa ni sehemu ya Mapambano juu ya swala hilo.
,,kwahiyo
likija suala la kupimwa ili kuwabaini wanaojihusisha na masula ya ushoga sisi
viongozi wa Dini wa kiislamu viongozi wa Dini ya kikirsto tujitokeze twende
tukapime ili pumba na mchele ujulikane tunaweza tukachanganyikana kwa kupinga
ushoga kumbe wewe mwenyewe ni shoga’’amenena Shekhe Mashaka
Hamisa
Saburi moja ya waumini walishiriki katika swala hiyo amesema Hotuba ya Shekhe
imegusa uhalisia wa namna mambo yalivyo katika kupambana na ushoga na kuiomba
serikali kuendelea kulipinga jambo hilo na kuongeza ufatiliaji wa mienendo ya
watoto waliopo majumbani na Mashuleni.
‘’Kama
mimi mzazazi hotuba ya shekhe nimeilewa nilikuwa naishauri serikali ifatilie
hasa katika watoto wa kike nawakiume pia hata sisi wazazi tunapokuwa nyumbani
inatakiwa tuwape Darasa watoto wetu tukiwa kama wazazi kuhusiana na haya mambo
ya ukatili’’amesema Hamisa
Sikukuu
ya Eid el Fitri huadhimishwa kila mwaka duniani kote ikiwa ni Sherehe ya kumalizika kwa mfungo mtukufu wa mwezi wa
Ramadhani ikiwa ni nguzo ya nne katika Dini ya kiislamu.