UZALISHAJI WA TUMBAKU KUONGEZEKA KATAVI

  

 

Meneja wa Bodi ya Tumbaku Mkoa wa Katavi Genwin Swai akitoa maelezo kwa mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko wakati wa uzinduzi wa soko la Tumbaku wa Kampuni ya Mkwawa Leaf Tobbaco LTD

Na  Walter  Mguluchuma

  Katavi

Mkoa wa Katavi unatarajia kuongeza uzalishaji wa zao la Tumbaku  kwa msimu huu  kwa kuzalisha  jumla ya kilo   Milioni 15. 5  ambazo  zitazalishwa  kutokana  na ekta   11,092 zilizo limwa  kwa msimu wa kilimo 2022/2023   uzalishaji wa msimu uliopita ulikuwa ni kilo  milioni 6.6 .

Mkurugenzi wa Mkwawa Leaf LTD Ahmed Mansoor Huwel amewahakikishia wakulima wa zao la Tumbaku mkoa wa Katavi kuwa kampuni hiyo itanunua zao la Tumbaku yote kwenye vyama vya Msingi ambavyo vimeingia mkataba wa ununuzi na Kampuni hiyo.
Mkoa wa Katavi unatarajia kuongeza uzalishaji wa zao la Tumbaku  kwa msimu huu  kwa kuzalisha  jumla ya kilo   Milioni 15. 5  ambazo  zitazalishwa  kutokana  na ekta   11,092 zilizo limwa  kwa msimu wa kilimo 2022/2023   uzalishaji wa msimu uliopita ulikuwa ni kilo  milioni 6.6 .

 Hayo yameelezwa na Meneja Mkoa wa Bodi ya  Tumbaku Tanzania  Genwin Swai  wakati atowa  taarifa  ya maendeleo  ya kilimo  cha  Tumbaku  Mkoa wa Katavi  wakati wa ufunguzi wa ununuzi wa soko la Tumbaku wa Kampuni ya ununuzi wa Tumbaku ya MKWAWA  LEAF TOBACCO     LIMETED uliofanyika katika chama cha Msingi Nsimbo Wilaya ya Mpanda .

Amesema kuwa  msimu wa kilimo  2021/2022 makisio ya awali  ya uzalishaji  yalikuwa ni kilogramu  8,220,000 hata hivyo hadi kufikia msimu wa kilimo ulipo malizika  ziliweza kununuliwa kilogramu   6,663,136 zenye thamani ya  shilingi Bilioni  26 madeni ya pembejeo yalikuwa Bilioni 13. 9 hivyo wakulima baada ya kulipa deni la pembejeo  walibaki na fedha kiasi cha shilingi Bilioni  12,035,185 293.

 Jumla ya vyama   vya msingi kumi na tano  vilishiriki kwenye uzalishaji huo na makampuni ya  Premium  Active  Tanzania na Mkwawa   ndio yaliyonunua tumbaku hizo za wakulima kwenye maeneo wanayolima zao hili la Tumbaku .

 Swai amebainisha kuwa  kwa msimu  huu wa kilimo wa 2022/2023 zoezi la ukaguzi  na tathimini  ya wingi  na ubora  wa zao la taumbaku ulifanywa mashambani  imebainika  kuwa eneo  la hekta  9,516 zilipandwa tumbaku  ambazo  zinatarajia kuzalisha kilogramu  11.696,853.

Amezitaja  baadhi ya changamoto zilizopo  kuwa  ni baadhi ya wakulima  kuendelea  kuchanganya  tumbaku  ambapo tumbaku yenye uzito wa juu huchanganywa na tumbaku  yenye ubora wa chini  ili kudanganya wanunuzi  au kuchanganya vitu   visivyo tumbaku (Ngulai)

Pia baadhi ya  vyama  kushindwa kulipa madeni  ya mikopo ya pembejeo na kushindwa pia kuwalipa wakulima  kutokana na vyama hivyo  kutofikia malengo  ya kulipa madeni yao kwa asilimia mia moja .

Mkuu wa Mkoa wa Katavi  Mwanamvua Mrindoko amewahimiza  watumie  wakutumia furua zilizoletwa na Serikali za kuwaletea wakulima ushindani  wa wanunuzi  hivyo wazitumia vizuri  furusa   hiyo  kwa kuwa waaminifu na waachane na tabia ya kuchanganya tumbaku yao na vitu ambavyo sio tumbaku .

Amewaonya wakulima  kuacha tabia  ya  kutorosha tumbaku kwani imekuwa  ni changamoto kubwa katika Mkoa wa Katavi  kwani  kwa watakao bainika na kukamatwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo ya kutaifishwa tumbaku waliyokuwa wanataka kuitorosha .

Alisema kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya  Mkwawa Amhed  Mansoor Huwel  amemwakikishia kuwa kampuni yake itakuwa inalipa  fedha kwenye chama husika ndani ya saa 24 mara baada ya kuwa amenunua Tumbaku  kwenye chama husika siku hiyo .

Mkurengezi wa Kampuni ya Mkwawa  Leaf  Tobacco  Limeted  Amhed  Mansoor  Huwel  ameeleza kuwa kampuni hiyo imekuja kununua tumbaku huku ikiwa na lengo la kumwinua mkulima kuanzia wa chini hadi wa juu kwani wapo tayari kununua tumbaku yote ambayo itakuwa imelimwa na mkulima .

Amefafanua kuwa Kampuni hiyo inafanya  shughuli ya ununuzi wa tumbaku kwenye mikoa 12  inayozalisha zao la tumbaku hapa  nchini  na kwa msimu huu wamepanga kununua kilogaramu  milioni 45nchi nzima na msimu ujao watanunua kilo milioni 90  ambapo msimu utakao fuata watanunua kilogramu milioni 130 ili kumkomboa mkulima aweze kujiongezea kipato chake .


Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages