Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akizungumnza na waandishi wa Habari ofisini kwake na kutuma salamu za Pasaka kwa wananchi wa mkoa wa Katavi. |
Waandishi wa habari mkoa wa katavi wakiwa katika majukumu yao wakati mkuu wa mkoa wa katavi akitoa salamu za Pasaka kwa wananchi wa mkoa wa katavi. |
‘’tusiondoke
kwenda kusherekea na kuacha Nyumba zetu zikiwa hazina aina yeyote ya ulinzi
kwakuwa kuna baadhi ya watu hutumia mwanya wa sikukuu hizi kufanya vitendo vya
wizi’’amesema Mrindoko.
Amesema
kuwa wazazi na walezi wawe walinzi kwa watoto wao ili kuepusha watoto hao
kupotea.
Katika
hatua nyingine amepiga marufuku watoto kwenda katika Maeneo ya Starehe kwenye
Mziki wa watoto maalufu kama [Disko toto ] kwa ni katika vipindi mbambali
kulisha wahi kutokea maafa yanayotokana na Mziki kwa watoto [Disko toto ]kwenye baadhi ya maeneo
hapa nchini hivyo nilazima kuchukua tahadhari.
‘’tulishawahi
kushuhudia Maafa kutokana na Mziki wa watoto, watoto wetu washerekee siku kuu
hii katika maeneo ya wazi ambayo yanatambulika ili kuepusha maafa yanayoweza
kujitokeza’’
Ametoa
tahadhari kwa watumiaji wa vyombo vya moto kuzingatia sheria za usalama barabarani ili
kuepusha ajali amabazo zinaweza kujitokeza katika kipindi hiki cha siku kuu ya
Pasaka.
Amewahakikishia wananchi kuwa mkoa umejipanga kuimalisha ulinzi katika maaeneo ya Ibaada wakati wa sikukuu ya Pasaka
Amewatakia wananchi wote wa mkoa wa Katavi kusherekea siku kuu ya Pasaka kwa amani na utulivu na mkoa wa Katavi upo salama