RC KATAVI AHIMIZA UWEKEZAJI WA KUCHAKATA MAZAO YA MIFUGO.

 

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akimkabidhi Mwenyekiti wa Kashaulili Amcos Charles Ngonyani Mashine ya kuchakata chakula cha mifugo.

Na Walter Mguluchuma -Katavi

Serikali ya Mkoa wa Katavi imewahimiza wawekezaji  wa ndani na nje wa mkoa huo kufungua viwanda vya kuchakata mazao ya mifungo ambapo vitachangia ukuaji wa uchumi pamoja nakumarisha Lishe kwa wananchi.

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akimkabidhi cheti cha usajili wa Kashaulili Amcos Charles Ngonyani.
Wito huu umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi  Mwanamvua  Mrindoko  wakati alipokuwa akikabidhi vifaa vya uchakataji wa mazao ya mifugo na vifaa vya kuhifadhia mifugo vilivyotoewa  na Rais Dkt  Samia  Suluhu Hassani  Chama cha ushirika cha Maziwa cha Kashaulili .

Amebainisha kuwa Mkoa wa Katavi kutokana na  sensa  ya  mifugo ya Mwaka 2022 Mkoa huu  unamifugo ya kutosha  unajumla ya mifugo zaidi ya laki nane kwamaana hiyo   viwanda vya kuchakata mazao ya mifugo  ninahitajika sana kutokana kuongezeka kwa mifugo kwa kasi kubwa kwani kwa sasa Mkoa unakisiwa kuwa na mifugo zaidi ya milioni  moja .

Mrindoko  amewataka wananchi  wa Mkoa huu  na nje ya Mkoa huu kufungua viwanda vya kuchakata  mazao ya mifugo kwani wawekezaji sio lazima wawe ni wazungu peke yao .

Amebainisha kuwa  Mkoa wa Katavi unahitaji   zaidi viwanda  vya chakata mazao ya  mifugo  kuanzia  nyama   ngozi  na maziwa  hivyo  chama hicho cha Ushirika wa maziwa  cha Kashaulili wahakikishe wanaanzisha kiwanda cha kuchakata mifugo .

Amesema  Mkoa wa Katavi unakiwanda kimoja tuu cha kuchakata maziwa  na hauna kiwanda hata kimoja cha kuchakata  mazao ya ngozi na chakula cha mifugo  na ndio maana ngozi   za mifugo mbambali zinaoza na kutupwa hivyo bado watu wanayofursa kubwa  ya kufungua viwanda kwenye Mkoa wa Katavi .

Kutokana na hali hiyo Serikali ipo tayari  kuendelea kuimarisha sekta ya mifugo kupitia mipango ya Rais Dkt Samia Suluhu  Hassan hivyo wanajitaji viwanda kwenye Mkoa huu

 Katibu  Tawala wa Mkoa wa Katavi  Abbas  Rugwa amesema  anaamini kuwa vifaa hivyo walivyokabidhiwa vitawafanya hapo baada kuwa na vifaa vingi zaidi  ya hivyo walivyopewa .

Ameeleza kuwa   huo ni mwanzo mzuri ambao  utawafanya watu wengine waweze  kuvutika na kuanzisha  viwanda vingine vya  kuchakata mazao ya mifugo kwenye Mkoa huu kutokana na mahitaji yalipo .

Mwenyekiti wa  ushirika wa maziwa  wa  chama cha Kashaulili  Charles Ngonyani amesema kuwa vifaa hivyo walivyokabidhiwa vitawafanya kuweza  kuwa na uwakika wa   kupata maziwa yenye ubora  na yaliyosalama zaidi .

Pia wanauhakika mifugo yao   kuanzia sasa  haitakuwa na shida ya  kula chakula ambacho  ambacho majani yake ambayo ni magumu kutoka na kuwepo kwa mashine ya kuchakata chakula waliopewa

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages