‘’Sisi kama jeshi la polisi
tumeanjiandaa kuimalisha ulinzi wa Rai na mali zao kuelekea kipindi hiki cha
Siku Kuu ya Eaid el Fitri niwahakikishie wananchi wa mkoa wa Katavi tutafanya
doria za kila aina ili kuhakikisha usalama kwenye siku kuu hii amesema Makame’’
Katika hatua nyingine kamanda Makame
amewaonya watumiaji wa vyombo vya moto kuelekea sikukuu ya Eid el Fitri
kuendesha vyombo vyao vya moto kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani.
‘’tuwaonye tena Madreva wa vyombo
vyamoto kutopakia uzito hasa Pikikipiki kutobeba Abiria zaidi ya mmoja hatutasita
kuwakamata na kuwapeleka mahakamani wale wote watakao bainika na makosa hayo’’
amesema Makame.
Pamoja na hayo amewaomba wazazi
kuwamakini na watoto wao kwa kutowaruhusu kwenda katika Maeneo ya starehe kwa
kulinda usalama wao ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na matukio yanayoweza
kujitokeza yenye sura ya upotevu wa watoto na kufanyiwa ukatili na unyanyasaji.
‘’Nimalufuku kumbi hizi za starehe
kuluhusu watoto wenye umri chini ya miaka 18 kuingia tutapita na kujilidhisha
kwenye kumbi hizi tukibaini kuna watoto wenye chini ya umri wa miaka 18
tutakukamata na kukupeleka katika vyombo vya sheria’’ amesisitiza Makame
Pamoja na hayo kamanda amewaomba wanachi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi mkoa wa Katavi kwa kutoa taarifa za waharifu na uharifu ili kuendelea kuimalisha ulinzi wa Raia na mali zao.