KAPUFI AIBUKA NA HOJA YA HUDUMA USAFISHAJI FIGO ITOLEWE KATAVI.

 

Mbunge wa Jimbo la Mpada Mjini Sebastian Kapufi akiuliza swali Bungeni kuhusu Huduma ya usafishaji damu itaanza lini katika mkoa Kapufi

Na walter Mguluchuma.

Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi ameibuka Bungeni  na kuomba huduma ya usafishaji wa Figo uanze kutolewa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Katavi.

Baadhi ya muonekano wa Majengo ya Hospital ya Rufaa mkoa wa Katavi.

Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi ameibuka Bungeni  na kuomba huduma ya usafishaji wa Figo uanze kutolewa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Katavi.

Hoja hiyo ameiibua jana Bungeni Mjni Dodoma wakati wa Kipindi cha maswali na Majibu alipouliza swali kwa Serikali .

Aliuliza ni li nilini serikali itaanzisha  huduma  ya usafishaji wa Figo katika hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi alihoji Mbunge Kapufi

‘’nashukuru Mh Spika kwa nafasi Je nilini serikali itaanzisha huduma hii ya usafishaji Figo katika mkoa wetu wa Katavi’’

Akijibu hoja hoja hiyo kwa niaba ya Serikali Naibu waziri wa Afya ,Dk Godwin Mollel amemhakikishia Mh Kapufi kuwa huduma hiyo itaanza kutolewa katika mkoa wa Katavi.

‘’ Mollel amesema Mh Spika kwenye Hospital yao mpya ya Mkoa wa Katavi tayari vifaa vimenunuliwa sasa hivi wapo kwenye umaliziaji wa eneo ambalo inatakiwa vifaa hivyo visimikwe’’

Amesema huduma hiyo ya usafishaji wa Figo itaanza Mara moja kwakuwa huku tayari Mashine ya Ct scane Rais Samia ameisha inunua na tayari imeshafika katika mkoa wa Katavi.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages