Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Shanwe Mustapha Mkimasa akiwa katika jengo la mahakama ya Mwanzo Shanwe Manispaa ya Mpanda lililoungua moto. |
Na Paul Mathias.
Katavi.
Mahakama ya Mwanzo Shanwe iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi imeungua moto usiku wa kuamkia leo.
Sehemu ya jengo la mahakama ya Mwanzo Shanwe lilivyo ungua moto |
Mahakama ya Mwanzo Shanwe iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi imeungua moto usiku wa kuamkia leo.
Mwenyekiti
wa Serikali mtaa wa Shanwe Mustapha Mkimasa amesema kuwa amepata taarifa ya
kuungua kwa jingo hilo kutoka kwa Mtoto wake.
‘’Mimi
nimeambiwa tu mtoto wangu akitoka kwenda uani akaniambia Baba mahakamani pale
kuna moto mkubwa unawaka pale nikasogea hadi eneo hilo kukuta moto unaendelea
kuwaka ’’ amesema Mkimasa
Ameeleza
kuwa baada ya kufika eneo hilo alichukua jukumu la kutoa taarifa kwenye jeshi
la zimamoto na uokoaji wakati huo wananchi walikuwa wanaendelea kuuzima moto
huo.
Amebainisha
jeshi la zimamoto na uokoaji walipofika katika eneo la tukio walianza mara moja
kuuzima moto huo kwa ushirikiano mkubwa na wananchi walifika kwenye eneo la
tukio hilo.
Mustapha
amesema kwa namna ya moto huo ulio ugunza jingo hilo kuna nyaraka nyingi za
serikali zitakuwa zimeungua.
‘’Kwanguvu
yetu tumewajibika akina baba akina mama tumesaidia sana hili jengo lakini
inaonekana nyaraka nyingi za serikali zimeungua amesema ‘’Mustapha
Kamati
ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Katavi ikiongozwa na mkuu wa mkoa wa Katavi
mwanamvua Mrindoko imefika eneo la tukio na uchunguzi wa tukio hilo ukiwa
unaendelea.
Kwa habari zaidi endelea kutembelea ukurasa wetu wa
kataviclub.blogspot.com.