USAFI WAANZA KUFANYIKA ENEO WALILO LALAMIKIA WANANCHI


Usafi ukiendelea kufanyika katika eneo la Nyuma ya Ukumbi wa mikutano wa Idara ya Maji Mpanda Manispaa

Na Walter Mguluchuma.

Katavi,

Eneo la  ukumbi maarufa wa  mikutano ulipo kati kati ya   Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi  unao milikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika  eneo ambalo likuwa linalalamikiwa  na wananchi kwa kuhofia usalama wao kutokana na  kuwa kichaka limeanza kufanyiwa usafi .

Muonekano wa Eneo la ukumbi wa mikutano Idara ya Maji kabla ya kufanyiwa usafi 

Eneo la  ukumbi maarufu Idara ya Maji  wa  mikutano ulipo kati kati ya   Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi  unao milikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika  eneo ambalo likuwa linalalamikiwa  na wananchi kwa kuhofia usalama wao kutokana na  kuwa kichaka limeanza kufanyiwa usafi .

Mmoja wa wananchi wa Manispaa ya Mpanda Ally  Juma amepongeza hatua hiyo ya eneo hilo kufanyiwa usafi kwa kile alichoeleza kuwa likuwa linahatarisha usalama wa wananchi kutokana na kichaka kikubwa kilichokuwepo  kwenye eneo hilo .

muonekano wa usafi ukiendelea kufanyika 

Amesema kuwa kutokana hali  iliyokuwepo kwenye eneo hilo ilikuwa inasababisha  mji wa  Mpanda  kuonekana kuwa hauko katika hali ya usafi  kutokana na eneo hilo  kuwa lipo kati kati ya Mji .

Hatua hii  ya kufanyiwa usafi kwenye eneo hili umekuja ikiwa ni siku chache tuu baada ya wananchi kupitia chombo hiki kulalamikia eneo hilo kutaka kuhatarisha usalama wa wananchi  kutona na eneo hilo kuwa na kichaka cha nyasi ndefu 

Hatua hii iende sambamba na wananchi kuhamasishwa wananchi kuendelea kufanya usafi kwenye maeneo yao ya usafi na maeneo ya taasisi za Umma na Binafsi.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages