WANNE WAKAMATWA NA MENO YA TEMBO YENYE THAMANI TSH MILION 247

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi,Ali Hamad Mkame akionyesha meno ya Tembo yaliyo kamatwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi.

Na Walter Mguluchuma 

Katavi,

Jeshi la Polisi  Mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi wamewakamata watu wanne wakiwa na meno ya Tembo vipande 13 yenye thamani ya  zaidi ya shilingi Milioni 247.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi,Ali Hamad Makame akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake mapema leo.

Jeshi la Polisi  Mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi wamewakamata watu wanne wakiwa na meno ya Tembo vipande 13 yenye thamani ya  zaidi ya shilingi Milioni 247.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Ali Hamad Makame  amewaambia wandishi wa Habari  watuhumiwa hao wamekamatwa  katika maeneo mawili  tofauti .

Katika tukio la kwanza  watuhumiwa watatu  Alex Ruben(45) Mkazi wa  Kijiji cha Kapalamsenga Wilaya ya Tanganyika ,Masele  Kasema(36) Mkazi wa Kijiji cha Sitalike  Wilaya ya Mpanda na  Nkamba  Ntemula (45) Mkazi wa Maji Moto  Wilaya ya Mlele  walikamatwa wakiwa na vipande  saba vya meno ya Tembo .

Kamanda  Makame amesema  watuhumiwa hao wamekamatwa na meno  hayo ya tembo  huko katika Mtaa wa Ikulu  Kata ya Kawajense Manispaa ya Mpanda wakiwa wameyahifadhi ndani ya nyumba  kwa  ajiri ya kuyauza .

Maneno Peter mhifadhi Mwandamizi kaimu kamishina msaidizi hifadhi ya Taifa Katavi akitoa maelezo kuhusu meno ya tembo yaliyokamtwa.

Watu  humiwa hao wamekamatwa  kufutia jeshi la polisi na  Askari wa  Hifadhi ya Taifa ya Katavi  kuwa wamepata taarifa juu ya watuhumiwa hao  kujihusisha na maswala ya ujangili .

Amesema katika tukio  la pili Askari wa  Tanapa   kwa kushirikiana waliweza kumkamata mhumiwa   Michael Kisiba Mkazi wa  Sumbawanga  akiwa na vipande vya meno ya tembo  vipande 11 ambavyo ni sawa na  tembo  sita .

Amebainisha kuwa  mtuhumiwa huyo alikamatwa na men hayo ya tembo  huko katika eneo la  Kata ya Usevya kufuatia msako mkali uliofanywa wa kuwasaka watu wanao jihusisha na maswala ya ujangili .

Ameeleza kuwa Kisiba alikamatwa na meno hayo ya tembo  wakati akiwa  ameyahifadhi   ndani ya  mfuko wa  salifeti ambapo alikuwa ameyaficha  kwenye  kichaka .

Mhifadhi  Mwandamizi  wa  Hifadhi ya Taifa ya Katavi  Kamishina  msaidizi  Maneno  Peter   amesema kuwa idadi  ya meno hayo ya tembo ni sawa na tembo saba wenye thamani  ya Tshs 247.590 000 kwa fedha za Kitanzania .

Amesema vitendo hivyo vya watu   kujihusisha na vitendo vya ujangili ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi na nje ya Hifadhi watambue kuwa maeneo hayo siyo salama kwao.

Ameonya kuwa kuna shughuli nyingi za kufanya hivyo kwa mtu yeyote ambae atakae jihusisha na   maswala ya ujangili    atashughulikiwa kwa mijibu wa sheria hivyo ni  vema wakajihushisha na biashara halali  kama za kilimo na sio  kufanya ujangili

Kamishina  msaidizi  Maneno Peter amesema kuwa kukamatwa kwa meno hayo ya tembo  kutokana na juhudi ambazo wamekuwa wakizifanya za kuzuia ujangili  kabla ya kutekelezwa na wamekuwa wakifanya hivyo na kuwakamata watu kabla ya kufanya ujangili na baada ya kufanya ujangili . 

Kwa habari zaidi Tembelea ukurasa wetu wa 

kataviclub.blogspot.com

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages