Muonekano wa Nyasi Ndefu ambazo hazijafyekwa katika eneo la ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Maji Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi |
Na Walter Mguluchuma
Mpanda .
Baadhi ya Wananchi wa Manispaa Mkoani Katavi wameilalamikia
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kwa kushindwa kusimamia usafi wa mji hali
ambayo imewafanya kuhofia hali ya usalama wao kwa kushindwa kusimamia usafi na
Kuluhusu kuwepo kwa nyasi ndefu iliwepo eneo la nyuma ya ukumbi wa mikutano wa
Idara ya Maji unao milikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika .
Muonekano wa Nyasi Eneo la Nyuma ya ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Maji Mpanda Mjini
Baadhi ya Wananchi wa Manispaa Mkoani Katavi wameilalamikia Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kwa kushindwa kusimamia usafi wa mji hali ambayo imewafanya kuhofia hali ya usalama wao kwa kushindwa kusimamia usafi na Kuluhusu kuwepo kwa nyasi ndefu iliwepo eneo la nyuma ya ukumbi wa mikutano wa Idara ya Maji unao milikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika .
Mmmoja wa wananchi hao Peter Michael amesema kuwa wamekuwa wakipita kwenye eneo hilo nyuma ya ukumbi huu hata mchana huku akiwa na hofu ya usalama wake kutokana na kichaka kikubwa cha nyasi kilichopo maana mpaka kinaziba barabara .
Amesema licha ya kuwa eneo hilo lipo katika kati
ya Manispaa ya Mpanda lakini mtu unaweza ukakabwa hata mchana
kama muda huu unaopita hakutakuwa na mtu mwingine anae pita kwenye eneo .
Maiko Msanja amesema kuwa yeye huwa anashangaa kila anappopita
kwenye eneo hilo na kuona likiwa na kichaka tena kati kati ya mji
utadhani hakuna mamlaka ambazo zina wajibu wa kusimamia mazingira ya usafi .
Amebainisha kuwa mbaya zaidi ikitokea umepita usiku kwenye eneo
hilo linakuwa linatisha sana utadhani kama vile umefika eneo la msitu wa
Ntongwe Magharibi au kwenye Hifadhi ya Taifa ya Katavi .
Alitowa mfano wa kuwepo na tabia ya kwenye maeneo
yanayomilikiwa kiwa na Serikali kuwa kama yametelekezwa ni kama
siku za nyuma aliwahi kupita kwenye nyumba aliyokuwa
akiishi Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe
Mhando iko katikati maeneo ya Kotazi alivyoiona ni kama
imetekelezwa kutoka na mazingira yalipo kwenye eneo hilo.