Vijana katika mkoa wa Katavi wameaswa kuchangamkia Fursa za Vijana zinazo tolewa na serikali kwa kuunda umoja na kusajiliwa kisheria na Bodi ya wakandarasi ili waweze kupata kazi ndogo ndogo zinazotolewa na serikali kupitia wakala wa Barabara Tanrods Katika mkoa wa Katavi.
Vijana katika mkoa wa Katavi wameaswa kuchangamkia Fursa za Vijana zinazo tolewa na serikali kwa kuunda umoja na kusajiliwa kisheria na Bodi ya wakandarasi ili waweze kupata kazi ndogo ndogo zinazotolewa na serikali kupitia wakala wa Barabara Tanrods Katika mkoa wa Katavi.
Ushauri
huo umetolewa na Meneja wa Tanrods Mkoa wa Katavi Mhandisi Martin Mwakabende
alipotembelewa na Viongozi wa Jukwaa la Vijana Mkoa wa Katavi Ofisini kwake leo
Mwakabende
amesema katika sera ya Wizara ya Ujenzi kwenye Bajeti za Mkoa Asilmia 30
Hutegwa kwaajili ya Makundi Maalamu ambayo ni Wazee,Wanawake ,walemavu na
Vijana ambapo makundi haya huyalazimu kusajiliwa katika Bodi ya Wakandarasi na
baadae hatua zingine za kuomba miradi hiyo hufuata.
‘’hii
ni Sera ya wizara ya Ujenzi katika Bajeti inayopangwa na mkoa Asilimia 30
inabidi zitengwe kwaajili ya makundi maalumu kuna kundi la wazee,kundi la
Vijana,kundi la akina mama na kundi la wenye ulemavu makundi haya yote yanaweza
kuunda umoja wao na Kusajiliwa katika Bodi ya Wakandarasi hapo sasa wanakuwa na
kazi ya kuomba kazi za kufanya’’amesema Mwakabende
Amesema
katika Mwaka wa fedha ujao Tanroads
katika mkoa wa Katavi wanatalajia kuwa na kazi ndogo ndogo 16 ambapo
zitahusisha makundi hayo kwa kuangalia Mahitaji ya kazi kulingana na uhitaji
katika miradi husika.
‘’katika
mwaka wa Fedha ujao tunategemea kuwa na kazi ndogo ndogo 16 nahizi tumejaribu
kuziweka katika maeneo tofautitofauti tumetenga kazi Fulani zitafanywa na kundi
la vijana kwa mfano mwaka huu tumetenga aina tatu za kazi zitakazofanywa na
Makundi ya Vijana hii ni fursa kwa Vikundi vilivyosajiliwa na bodi ya
wakandarasi katika mkoa wa Katavi kuingia katika Mifumo hususani Taneps
kuangalia kazi zilizotangwa na Tanroads mkoa wa Katavi’’
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Jukwaa la kuwakomboa vijana Mkoa wa Katavi Saimon
Jonh amesema kuwa adhima ujio wa viongozi wa Jukwaa la vijana katika ofisi za
Tanrods Katavi ni kutambua mchango wa Tanrods namna inavyoshrikiana na na
jukwaa la vijana katika kushirki kazi ndogo ndogo za uelimishaji wa jamii
unaofaywa na jukwaa la vijana kwa
wananchi kwenye maeneo ambayo miradi hiyo ya Tanrods inapojengwa.
‘’sisi
kama jukwaa la Vijana mkoa wa Katavi tunashukuru namna ofisi yako imekuwa
ikitupa ushirikiano katika majukumu yetu hasa kwenye miradi hii midogo midogo
ambayo tumekuwa tukiipata kwa kutoa elimu ya maambukizi ya Virusi vya ukimwi
kwenye baadhi ya Miradi hapa mkoani kwetu’’amesema Saimon
Katika
hatua nyingine Jukwaa la kuwakomboa vijana mkoa wa Katavi limetoa cheti cha
Shukurani Kwa ofisi ya Tanrods Mkoa wa Katavi kwa kutambua mchango unaotolewa
na ofisi hiyo katika kwenye uelimishaji wa jamii kuhusu VVU na Ukimwi kwenye
baadhi ya maeneo ambayo miradi mbalimbali ya ujenzi wa Barabara hufanyika.