Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akiwahutubia wananchi katika kilele cha Siku ya wauguzi duniani yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Shule ya Msingi Kashaulili |
Na Paul Mathias
Katavi,
Wauguzi katika Mkoa wa
Katavi wameobwa kuendelea kufanya kazi kwa Weledi kwa kuzingatia miiko ya
Taaluma kwani wao ni Sehemu mhimu kwa kuokoa Uhai kwa Binadamu katika kazi zao.
Akiwahutubia wananchi wa
Mkoa wa Katavi kwenye kilele cha siku ya Wauguzi Duniani yaliyofanyika kimkoa katika
viwanja vya Shule ya Msingi Kashaulili Manispaa ya Mpanda , Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua
Mrindoko amesema kada ya wauguzi ina umuhimu Mkubwa jamii kwakuwa wao wamekuwa
sehemu ya kuponya maradhi kwa mwanadamu yanapo Mpata.Baadhi ya Wauguzi katika halmashauri ya Manispaa ya Mpanda wakiwa katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya Wauguzi Duniani
‘’baada ya Daktari kumaliza kazi yake ya
kuandika ni namna gani apate Matibabu anaendelea nae kwenye hatua za mbele kule
ni Muuguzi kwa maana hiyo Sekta hii kada hii ya Wauguzi wa aina zote ni mhimu
sana katika sekta ya Afya’’ amesema Mrindoko
Amesema kazi kubwa
inayofanywa na wauguzi kwa kuwaangali wagojwa kwa upole ni sehemu kuhakikisha
wanafanya kazi yao kwa kuzingatia maadili na weledi kwa Wagojwa wanaowahudumia
kwenye Zahanati,Vituo vya afya,Pamoja na hospitali ambapo kwa mwaka wa fedha wa
2022/2023 Mkoa wa Katavi ulipatiwa wafanya kazi 290 kwa mkoa wa katavi.
‘’niwapongeze sana tuendelee kuthamini kazi inayofanywa na wauguzi kwakuzingatia kuwa kundi hili ni kundi kubwa kwenye sekta ya utoaji wa huduma za afya kwenye hospitali zetu’’
Katika hatua nyingine
Mkuu huyo wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amsema kumekuwa na ongezeko la
Vituo vya kutoa huduma za upasuaji kwa mama
wajawazito kutoka 3 mwaka 2017 na kufikia 12 kwa mwaka 2023.
Awali akisoma Risala kwa
Mkuu wa Mkoa Mratibu wa TANNA Mkoa wa Katavi Augusta Thomas amesema kuwa kwa
sasa mkoa wa Katavi unawauguzi wapatao 403 waliosajiliwa idadi ambayo haiendani
na uhalisia wa Miundombinu ya afya iliyopo na kuimba serikali kuendelea
kuwekeza nguvu kazi katika Rasilimali watu hususani waauguzi.
Augusta ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuwaboreshea Miundombinu ya kufanyia kazi ikiwemo hospitali,pamoja n vituo vya afya.
Kwa upande wake Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda Paul Swakala amesema kuwa pamoja
uchache wa watumishi waliopo katika hospitali hiyo wafanyakazi hao wamekuwa
wakifanya kazi zao kwa kujituma nakwa weledi wa hali ya juu.
Maadhimisho ya kilele cha siku ya wauguzi Duniani 2023 yamebebwa na kaulimbiu inayosema WAUGUZI WETU MSTAKABALI WA MAISHA YETU.