Katavi
Kampuni ya ununuzi wa zao la Tumbaku ya Mkwawa Leaf Tobbaco imesema msimu wa kilimo wa wa 2022/2023 inatalajia kununua Kilo Millioni 45 za tumbaku Nchi nzima kwa vyama vya Msingi walivyofunga navyo Mkataba wa ununuzi wa zao la Tumbaku.
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akisaini Moja Bello Tiketi ya Mtumba wa Tumbaku kama ishara ya kuanza Rasmi kwa Masoko ya Tumbaku katika mkoa wa Katavi |
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mkwawa leaf Ahmed Mansoor Huwel wakati wa uzinduzi wa Masoko kwa Kampuni hiyo ulifanyika katika Kijiji cha Mtakuja Halmashauri ya Nsimbo mkoa wa Katavi amesema kuwa wao kama Mkwawa Leaf Tobbaco LTD wamekuja Kumkomboa mkulima kwa kununua Tumbaku zote Kwa vyama vya Msingi walivyoingia navyo mkataba wa ununuzi wa zao hilo.
‘’Ahamed anasema nataka kuwathibitishia Mkwawa ilipoanza Mwaka
jana Mh Mkuu wa Mkoa Makampuni yote yalikuwa yanatoa Makisio lakini Mkwawa
tumekuja na Staili Moja tunayo sema kwamba lima kwa uwezo wako kwani soko letu
ni Kubwa amesema ‘’Ahamed
Amesema kuwa kwa Msimu wa Mwaka jana Kampuni hiyo ilinunua
Tumbaku Milion Saba na Nusu huku Mwaka huu wakiwa na Mkataba wa Kununua Tumbaku
kilo Milioni Arobaini na Tano Nchi kiwango ambacho ni kikubwa kuliko Makampuni
mengine.
‘’Mwaka jana tulianza kwa kununua Milioni Saba na nusu,Mwaka huu tunamikataba ya kununua Kilo za Tumbaku Milioni 45 kiwango ambacho nikikubwa kuliko Makampuni yaliyotutangulia,,
Mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Mrindoko akiwa Mgeni Rasimi
katika Uzinduzi huo amewaomba wakulima kuwa waaminifu kwa kutochanganya na vitu
ambavyo haviendani ili kuongeza uzito wa Tumbaku kwenye Mitumba yao.
‘’Niwaombe wakulima kuiwa waaminifu kunachangamoto imetajwa hapa
kuna baadhi ya wakulima huchanganya Tumbaku na vituambavyo siyo sahihi ili
kuongeza uzito niwaombe wakulima kuwa waaminifu ‘’
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa wa Katavi Mwanamvua
Mrindoko amesema kuwa zao la tumbaku linaendeshwa kwa kanuni na taratibu hivyo
lazima zao hilo lisimamiwe vilivyo kwakuwa huchangia Mapato kwa halmashauri
kupitia ushuru wa zao hilo.
Wananchi waliohudhiria uzinduzi wa Masoko ya Tumbaku kwa Kampuni ya Mkwawa leaf Tobbaco uliofanyika katika kijiji cha Mtakuja Halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi. |
Salehe Maduhu Mkulima wa zao hilo katika Kijiji cha Mtakuja
amesema kuwa tangu Kampuni hiyo ya Mkwawa ianze kufanya kazi katika msimu
uliopita wamekuwa na matunini nayo kwenye ununuzi wa zao hilo la Tumbaku.
Mkoa wa Katavi unajumla ya Vyama vya Msingi 20 vinavyoshiriki kilimo cha zao la Tumbaku kwa Msimu wa Kilimo wa 2022/2023 ambapo Mkoa wa Katavi unatalajia kuzalisha Kilo za Tumbaku Milioni 11 ,696,853.