Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Faustine Maijo akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari ya utendaji kazi wa taasisi hiyo kwa kipindi cha Mwezi January March |
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Katavi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi kwa kipindi cha robo mwaka ya Aprili hadi june 2023 inatarajia kuimarisha juhudi za kuzuia Rushwa kwa kukagua miradi ya maendeleo kwa kuwahamasisha wananchi na kutoa elumu ya ushiriki wa wananchi kuzuia Rushwa
Waandishi wa habari mkoa wa Katavi wakiendelea na Majukumu yao wakati mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Faustine Maijo alipotoa taarifa ya utendaji kazi kwa mwezi January hadi March.
Katavi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi kwa kipindi cha robo mwaka ya Aprili hadi june 2023 inatarajia kuimarisha juhudi za kuzuia Rushwa kwa kukagua miradi ya maendeleo kwa kuwahamasisha wananchi na kutoa elumu ya ushiriki wa wananchi kuzuia Rushwa
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Faustine Maijo wakati akitowa taarifa ya utekelezaji wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu ya kuanzia mwezi Machi hadi mwezi june 2023.
Amesema Takukuru Mkoa wa Katavi inatarajia
katika kipindi hicho kuimaimarisha
juhudi za Kuzuia Rushwa kwa kukagua miradi ya maendeleo ,kuimarisha na kutoa
elimu ya kushiriki wananchi
katika kuzuia Rushwa kupitia
nyenzo mbalimbali .
Pia watatumia uelimishaji
katika mikusanyiko mbalimbali kwa kutumia mwongozo
wa TAKUKURU RAFIKI na pia wataendelea kufatilia
kwa karibu fedha zote zinazotolewa na Serikali zikiwepo
fedha za mradi
wa Boost ili kuhakikisha zinatumika
kama ilivyokusudiwa na kuonyesha
thamani ya fedha .
Vilevile
wataendelea kufatilia makusanyo
na uwasilishaji wa mapato
yanayotokana na mashine za POS
na kuchukua hatua stahiki
kwa wale watakaobainika kufuja
mali za umma ikiwemo wanao tumia
fedha mbichi .
Maijo ameeleza kuwa
Takukuru kwenye kipindi
hicho watafanya warsha
na wadau kujadili matokeo
ya uchambuzi za mifumo zilizokamilika ili
kuweka maazimio ya namna bora
ya kuziba mapungufu yaliyobainishwa katika uchambuzi hizo .
Aidha
watafanya uchunguzi wa
haraka kwa taarifa zote zitakazopokelewa na ambazo
uchunguzi wake unaendelea
ili ziweze kukamilika mapema .
Kuhusu
malalamiko ya Rushwa Takukuru
Mkoa wa Katavi wameendelea kupokea malalamiko
yanayohusiana na vitendo vya
Rushwa ambapo katika kipindi hicho
wameweza kupokea malalamiko 51 kati ya malalamiko hayo malalamiko
35 yalikuwa yanahusu Rushwa na
malalamiko 16 hayakuwa yanahusiana na Rushwa .
Maijo ametowa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Katavi kutowa taarifa za vitendo vya Rushwa pindi vinapokuwa vimetokea .