CHADEMA, KATIBA MPYA KUBANA WIZI FEDHA ZA UMMA

Mwenyekiti wa chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA Taifa Freeman Mbowe akiwahutubia wanachama na wananchi wa Mkoa wa Katavi.[Picha na George Mwigulu]

Na Paul Mathias,Katavi

Chama cha Democeasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa kitaendelea kusimamia misingi ya Chama hicho kwa kutetea Haki,Uhuru, na Democrasia  kwa wanachama wa chama hicho na wananchi wa Taifa la Tanzania.

Wanachama wa chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa katavi waliojitokeza katika mkutano uliohudhuriliwa na viongozi wa Chama hicho Taifa katika viwanja vya Shule ya Msingi Kashato Mpanda Mjini.[Picha na George Mwigulu]

Chama cha Democeasia na Maendeleo Chadema kimesema kuwa kitaendelea kusimamia misingi ya Chama hicho kwa kutetea Haki,Uhuru, na Democrasia  kwa wanachama wa chama hicho na wananchi wa Taifa la Tanzania.

Akiwa hutubia wanachama wa Chama hicho katika uzinduzi wa Opearesheni 255 katika mkoa wa Katavi kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Kashato Chenye lengo la kufikisha ujumbe kwa wanachama kuhusu takwa la katiba Mpya.

Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Freeman Mbowe amesema kuwa chama hicho kinahitaji Katiba Mpya kwakuwa ni hitaji lao kwa suluhu ya changamoto mbalimbali 

Mbowe amesema kuwa chama hicho kinaamini katika Misingi yake ya Haki,Uhuru,Democrasia na Maendeleo kwa maendeleo ya Chama hicho na Taifa kwa ujumla.

‘’Mbowe anasema Wajibu wangu Mkubwa leo kwenu nikusisitiza Misingi ya Chama chetu ili tuweze kufikia malengo yetu  tuwe na chama imara zaidi chama kiunganishi kinachounganisha watanzania wote wanaopenda Haki’’

Ameeleza kuwa chama hicho kitaendelea kuamini katika Misingi hiyo ili kuweza kufikia malengo yake ya kushika Dola kwakuwa chama hicho bado kimebakia kuwa tumaini la Watanzania katika kuleta Mabadiliko ya kweli.

‘’tunawashukuru sana wananchi bila ninyi hatuwezi kuwepo tumeendelea kusisimama tukijua kwamba tunaongoza Mamilioni ya watanzania wanao penda taifa lenye Haki asanteni kwa kuwa Mashujaa asanteni kwa kusimama na sisi asanteni kwa kuvumilia lakini kesho yetu inaweza kuwa bora ‘’amesema Mbowe

Baadhi ya Wananchi wa Mkoa wa Katavi waliojitokeza kwa wingi katika Mkutano wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo katika viwanja vya shule ya Msingi Kashato Manispaa ya Mpanda wakati wa uzinduzi wa operation maalumu wa chama hicho 255. (Picha na George Mwigulu

Kuhusu katiba mpya amesema kuwa ili kuhakikisha haki inapatikana kwa wananchi Msingi mkubwa ni kupata katiba mpya itakayo tokana na wananchi.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara Tundu Lissu amesema kuwa takwa kubwa la chama hicho ni katiba mpya ambayo itaondoa Urasimu na Ubadirifu wa Mali za umma unaojitokeza kwa sasa.

‘’Mthibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali anatuambia kwamba katika mwaka huu mmoja wa fedha pekee yake fedha ambazo zimepigwa ni zaidi ya Trion Mbili kwa hiyo mimi sijawahiona hiyo trioni msiniulize mimi ikowapi ‘’amesema Lissu

Lissu amesema kuwa ili kuwa na Taifa lenye Umoja na Mshikamano lazima Katiba Mpya inayo tokana na Wananchi ipatikane.

Katibu Mkuu wa Chama hicho Taifa John Mnyika amesekuwa kwa muda sasa kumeshuhudiwa kupolomoka kwa sekta ya Kilimo kutoka asilimia 4.9 mpaka 3.9 hali hiyo ikisabisha Maisha ya vijijini kuwa Ngumu.

Opeseheni hiyo ya 255 itadumu kwa muda wa siku tatu katika mkoa wa Katavi kwa kutembelea Majimbo ya mkoa wa Katavi kwa lengo la kuangalia uhai wa chama na kupeleka ujumbe juu ya umuhimu kuhusu katiba Mpya.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages