Na Walter Mguluchuma
Katavi .
Wajumbe wa
Kamati za PETS za kutoka kwenye Vijiji vya Kasekese na Lugonesi vilivyopo katika Wilaya ya Tanganyika Mkoani
Katavi wamepatiwa mafunzo ya siku tano
yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Usevya Development Society [UDESO] mafunzo hayo kwaajili ya kuwajengea uwezo ili kusimamia rasilimali na miradi ya Maendeleo .
Mkurugenzi wa Taasisi ya Usevya Development Society[ UDESO] Eden Wayimba akitoa neno kwa washiriki wa Mafunzo. |
Wajumbe wa Kamati za PETS za kutoka kwenye Vijiji vya Kasekese na Lugonesi vilivyopo katika Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi wamepatiwa mafunzo ya siku tano yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Usevya Development Society [UDESO] mafunzo hayo kwaajili ya kuwajengea uwezo ili kusimamia rasilimali na miradi ya Maendeleo .
Mafunzo
hayo ya siku tano yaliyowashirikisha wajumbe wa PETS wa kutoka kwenye vijiji
vya Logonesi na Kasekese yamefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa
Kichangani uliopo Manispaa ya Mpanda Mafunzo hayo yamefungwa na Msajiri
Msaidizi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (TDC) wa
Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika
Halima Kitumba .
Kitumba
akifunga mafunzo hayo amesema washiriki
wa mafunzo hayo yamewafanya wawe wa mfano
kwenye maeneo mengine katika Halmashauri
hiyo kwa kuweza kuisaidia kupeleka
mgao wa
shughuli zote zinazo husiana na
miradi na rasilimali kwenda kwa uswa.
Amebainisha kuwa kabla ya kupatiwa mafunzo
hayo hapo nyuma ilikuwa ni tofauti kwa kuwa wasahivi tayari wametambua haki zao
na watakuwa na uwezo wa kwenda katika Halmashauri na kuhoji haki za mgawanyo kwenye Kata kuhusu mikopo na miradi.
Kitumba
amewasisitiza watihimu hao kutumia vizuri mafunzo hayo kwa kuhakikisha wanakwenda
kwenye vijiji vingine na kuwapatia elimu kama ambayo wamepewa wao na mwisho wa
siku kamati zitakapokuwa hai kwenye
vijiji vyote kwani watakuwa pia na uwezo
wa kuandaa mikutano ambayo itakuwa haija fanyika kwenye vijiji vyao na kuhoji bajeti za miradi mbalimbali ya maendeleo
ingawa kwa sasa wanaanza na miradi ya
elimu .
Washiriki wa Mafunzo wakiwa katika picha ya Pamoja na Mkurugenzi wa UDESO na Msajili Msaidizi wa Mashirika yasiyo kuwa ya KiserikaliWilaya ya Tanganyika Halima Kitumba . |
Amesema kuwa mafunzo hayo yalikuwa yamejikita kwenye maeneo makuu yafuatayo wameangalia
dhama nzima ya madaraka ya
Serikali ili kumezesha mwananchi katika ushiriki
nakusimamia rasilimali zote za
umma zinazopelekwa kwenye maeneo yao
Vilevile wameangalia
dhana nzima ya utawala bora ni namna gani ambavyo wananchi anapaswa kuwa sehemu ya ushiriki wa sehemu uhimizaji wa utawala bora
kwa kutambua umuhimu wa ihimizaji wa utawala bora
Mkurugenz
Mtendaji i wa shirika lisilo la
kiserikali la Usevya Development Sociaety(UDESO) Eden Wanyimba amesema kuwa
mradi huu katika Wilaya ya
Tanganyika unatekelezwa kwa
kushirikiana UDESO na Taasisi
ya WAJIBU .
Mradi huu unatekelezwa katika vijiji hivyo
viwili katika Wilaya ya Tanganyika ulianza mwezi machi 2023 na unajikita zaidi katika kuangalia utekelezaji
wa mapendekezo yaliyotolewa katika sekta ya elimu ya awali kupitia ripoti ya mdhibiti
na mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali CAG Mwaka 2017.