AGIZO LA RC LATEKELEZWA'' KIJIJI CHA DIRIFU WASOMEWA MAPATO

Afisa mtendaji wa Kijiji cha Dirifu Evirius Mathayo akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali katika mkutano wa kuwasomea mapato na matumizi wananchi wa Kjiji hicho.
Na Paul Mathias

Mpanda.


Wakazi wa Kijiji cha Dirifu Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wamewataka viongozi wa Kijiji hicho kuwa na utaratibu wa kuwasomea Mapato na matumizi ili kuongeza uwajibikaji kwa wananchi.

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Dirifu wakiwa katika mkutano wa hadhara wa kusomewa mapato na matumizi ya kijiji chao.

Wakazi wa Kijiji cha Dirifu Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wamewataka viongozi wa Kijiji hicho kuwa na utaratibu wa kuwasomea Mapato na matumizi ili kuongeza uwajibikaji kwa viongozi wa Kijiji hicho.

Wakiwa katika mkutano wa Hadhara uliofanyika katika ofisi za kijiji hicho wananchi hao wamesema kuwa kumekuwa na ukakasi kwa viongozi wa Kijiji hicho kutosoma  mapato na matumizi kwa wakati hali ambayo huzua wasiwasi juu ya Fedha za maendeleo zinazovyotumika kwenye Kijiji chao.

Emanuel Julias mkazi wa Kijiji cha Dirifu anaiomba serikali kupitia viongozi wa juu kuendelea kutia Msukumo kwa viongozi wa Kijiji hicho kuwa na utaratibu wa kuwasomea mapato na matumizi ili kufahamu uhalisia wa mapato yanayotokana na kijiji na halmashauri.

Wananchi wa Kijiji cha Dirifu wakifatilia kikao cha mapato na matumizi kijiji hapo

‘’tunahitaji vitu mhimu kwenye kijiji chetu ila kwa kusuasua sana hata ukifatilia mikutano hii tunayosomewa tunaipata kwa vurugu sana mpaka mpaka tubembelezane ndo tunasomewa mapato’’

Ameeleza kuwa kuna faida ya kusomewa mapato na matumizi kwenye kijiji ili kujua mahitaji ya kijiji na kuona namna bora ya kuwashauri viongozi ili kuleta maendeleo kijijini hususani miundo mbinu mbalimbali kama elimu,Afya,Maji na Barabara.

Salma Juma anasema kuwa utaratibu wa kusomewa mapato na matumizi unawasaidia wananchi kufahamu kilichopatikana na jinsi kinavyo tumika kwa wananchi kijijini hapo.

‘’mikutano ndiyo faida ya kujua mapato na matumizi tatizo la hiki kijiji kina mgawanyiko wajumbe wa serikali ya kijiji na wenyeviti wa kijiji hawahusishwi hali hii huwa inaleta shida katika suala la maendeleo ya kijiji chetu’’ anasema Salma

Wananchi wa Kijiji cha Dirifu wakijadiliaana mambo kadhaa wakati wa kikao cha Mapato na matumizi 

Mwenyekiti wa Kijiji cha Dirifu Jofley Maiko Mbogo amesema kuwa changamoto ya kutosoma mapato na matumizi kwa wakati inatokana na watendaji wengi katika kijiji hicho kuhamishwa mara kwa mara.

‘’tangu mwaka 2018 wakati nimekaimu kijiji nilikuwa napata changamoto ya watendaji yaani ukikaa na mtendaji ndani ya miezi mitatu hadi mitano analetwa mtendaji mwingine hadi sasa mtendaji nilie nae niwatano’’

Wananchi Kijiji cha Dirifu wakisikuliza taarifa ya Mapato na Matumizi kwenye mkutano huo 
Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo amebainisha kuwa atahakikisha wananchi wanasomewa mapato na matumizi ya kijiji chao kwa mujibu wa sheria ili kuongeza Imani kwa wananchi na viongozi wanaowaongoza.

Katika mkutano huo Mtendaji wa Kijiji hicho Evirius Mathayo amewasomea mapato na matumizi wananchi kwa mwaka wa 2022/ hadi May 2023 yenye Thamani ya shilingi Milion 11.

Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko alipofanya ziara ya kutatua mgogoro wananchi wa Dirifu na mwekezaji alitoa agizo la kuhakikisha wananchi hao wanasomewa mapato na matumizi

kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa

kataviclub.blogspot.com

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages