Msitahuki Meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry akifungua Kikao cha Baraza maalumu la Mdiwani la kujadili taarifa za Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali zinazoishia June 2022. |
Na Walter Mguluchuma
Mpanda.
Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imepongzwa kwa kuwa ni miongoni mwa Halmashauri hapa Nchini kwa kupata hati safi katika taarifa iliyotolewa na mkaguzi Mkuu wa Serikali kwa mwaka wa fedha 2021 na 2022 kutokana na utendaji kazi mzuri unaofanywa na Halmashauri hiyo .
Madiwani wa Manispaa ya Mpanda wakiwa kwenye baraza maalumu la kujadili taarifa za Mkaguzi na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali [CAG]
Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imepongzwa kwa kuwa ni miongoni mwa Halmashauri hapa Nchini kwa kupata hati safi katika taarifa iliyotolewa na mkaguzi Mkuu wa Serikali kwa mwaka wa fedha 2021 na 2022 kutokana na utendaji kazi mzuri unaofanywa na Halmashauri hiyo .
Pongezi hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti wakati wa
kikao maalumu cha Baraza
la Madiwani lililo kutana kwa
ajiri ya kujadili taarifa ya mkaguzi
mkuu wa Serikali iliyoishia June 2022 kikao hicho cha Baraza la Madiwani
kimefanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda na kuongozwa namstahiki Meya wa Manispaaya Mpanda hiyo Haidari Sumry .
Akiwatubia wajumbe wa Baraza hilo la Madiwani Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Hassan
Abas Rugwa ameeleza kuwa hayo wanayo yashuhudia kwenye Manispaa ya kupata hati safi inatokana
na ufanisi wa muunganiko wa Madiwani
pamoja na wataalamu .
Rugwa amewataka waendelee kusimamia pale waliposimamia na waendelee kubuni mikakati mipya na nzuri zaidi ya kuweza kuisimamia
Halmashauri ili Kuyafikia malengo ndani
ya Halmashauri.
Amefafanua kuwa pamoja na mafaniko hayo
zipo baadhi ya changamoto kwenye
baadhi ya maeneo ambazo zimewafanya wafike hapa kwa ajiri ya kujadili
changamoto hizo chache na wanao uwezo wa
kufanya hoja hizo hazijitokezi tena kwa
kuwa uwezo huu upo ndani ya Halmashauri yenyewe .
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akifatilia kwa Makini taarifa za Mkaguzi mkuu wa hesabu za wakati wa kikao cha baraza maalumu la Madiwani halmashauri ya Manispaa ya Mpanda |
Amesema watahakikisha wanaendelea kufanya kazi kwa
kushirikiana karibu na uongozi wa Serikali wa Wilaya na Mkoa na wako tayari kuendelea kupokea ushauli ili waendelea kufanya
vizuri katika usimamizi wa fedha na miradi ya maendeleo .
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamira Yusuph amesema kuwa ni faraja kwa Halmashauri hiyo
kuweza kupata hata safi hali hii inaonyesha kuwa kuna kazi kubwa imefanywa
kwenye Manispaa ya Mpanda.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa
kwenye kikao hicho ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo
Busweru amewataka wafanye kazi
kwa kuzingatia sheria na taratibu za manunuzi ili kuepukana hoja za CAG ambazo zinaweza kujitokeza .
Amewasisitiza wakusanye mapato kwa halali na kwa weledi mkubwa ili waweze kufikia malengo waliojiwekea na kuweza kuwahudumia wananchi kwa kuwatatulia changamoto zao .