Na Paul Mathias
Katavi,
Makamu mwenyekiti wa Chama cha
Democrasia na maendeleo CHADEMA Kanda ya Magharibi Masanja Katambi amesema
chama hicho kimeanza mikakati ya kujianda na uchaguzi wa Serikali za Mitaa
mwakani.
Makamu mwenyekiti wa Chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA Kanda ya Magharibi Masanja Katambi amesema chama hicho kimeanza mikakati ya kujianda na uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani.Katibu wa chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA Mkoa wa Katavi Almasi Ntije akihutubia mkuatano wa hadhara kata ya Kawajense Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi
Akiwa hutubia wanachama wa
Chama hicho katika Mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Chama hicho katika kata
ya Kawajense Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi.
Masanja amesema tayari mikakati
imeanza ya kuhakikisha Chama hicho Mkoa wa Katavi kinaenda kufanya vizuri
katika uchaguzi huo wa Serikali za mitaa .
‘’Kama Chama tunaomba mtuunge
mkono mwakani tunauchaguzi wa Vitongoji na Vijiji jiandikisheni kama wanachama
wa Chadema ili mgombee kwenye mitaa,Mgombee kama wajumbe hii itaweka Msingi
mzuri katika kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2025 ‘’amesema Masanja
Kupitia mkutano huo Masanja
ametangaza nia yake ya Kugombea Ubunge wa Jimbo la Mpanda mjini na kuwaomba
wanachi na wanachama wa chama hicho kukiunga mkono katika kuelekea chaguzi
zinazokuja katika siku za usoni.
‘’ningependa niwatangazie wana
Kawajense moja ya wanachama wa CHADEMA waliotangaza nia ya kulitaka Jimbo hili
la Mpanda Mjini katika uchaguzi ujao ni pamoja na mimi ila chama kitachuja ‘’
Almasi Ntije Katibu wa Chama
cha Democrasia na Maendeleo Chadema Mkoa wa Katavi amesikitishwa na baadhi ya
Watendaji wa Kata na Mitaa kwa kutosoma Mapato na matumizi kwa wananchi takwa ambalo nilakisheria
Amesema watakuwa na mwendelezo
wa mikutano ya hadhara kwa wananchi kwa lengo la kukijenga chama na kuwaamusha
wananchi juu ya mambo Mbalimbali na kuwaasa kuendelea kujiandikisha na kupatiwa
kadi za chama hicho kwenye Mfumo wa kisasa yaani electronic Systeam maalufu
kama Chadema Digital zoezi ambalo linaendelea kwa sasa.
Mkutano huo umehudhuliwa na
Viongozi mbalimbali wa chama hicho katika ngazi ya Mkoawa Katavi.
kwa habari zaidi tembelea ukuerasa wetu wa
kataviclub.blogspot.com