CRDB BENKI YASOGEZA HUDUMA NKASI

Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Peter Lijualikali [katikati]akikata utepe wa kuashiria kufunguliwa kwa Tawi la Benki ya CRDB Wilaya Nkasi Mkoa wa Rukwa.

Rukwa-Nkasi

 Na Paul Mathias

Wananchi katika Wilaya Nkasi Mkoa wa Rukwa wameombwa kuchangamkia fursa za Kibenki zinazo tolewa na Benki ya CRDB kwa ili kujikwamua kiuchumi.

Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Peter Lijualikali wa kwanza Kulia akiwa na Justo Ngwelo kaimu Mkurugenzi wa huduma kwa wateja kutoka Benki ya CRDB Makao makuu pamoja na meneja wa CRDB kanda ya nyanda za juu kusini wakifurahi jambo wakati wa uzinduzi wa Benki ya CRDB Wilaya Nkasi

Wananchi katika Wilaya Nkasi Mkoa wa Rukwa wameombwa kuchangamkia fursa za Kibenki zinazo tolewa na Benki ya CRDB kwa ili kujikwamua kiuchumi.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Peter Lijualikali wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tawi la Benki ya CRDB uliofanyika katika viunga vya Tawi la Benki hiyo Wilaya ya Nkasi.

Lijualikali amesema kuwa kufunguliwa kwa Tawi la Benki ya CRDB Wilaya ya Nkasi itakwenda kuinua uchumi kwa wananchi wa wilaya ya Nkasi kwa kuzingatia kuwa wakazi wa wilaya ya Nkasi asilimia 81 ni wakuliuma wa Mazao Mbalimbali.

‘’naamini kufunguliwa kwa tawi hili kutaongeza tija iwapo wakulima watapata mikopo inayotolewa na Benki ya CRDB tena kwa riba iliyo chini ya asilimia 10 ‘’ameeleza Lijualikali

Amesema sekta ya Fedha inamchango mkubwa katika Kusukuma maendeleo kwa wanamchi hivyo ni fahari kubwa kwa wananchi wa wilaya ya Nkasi kuwa na Tawi la Benki ya CRDB.

‘’inafahamika duniani kote kwamba sekta ya Fedha inayojumuisha Banki ndio msingi wa maendeleo ya kila anaetaka kufanikiwa kiuchumi’’

 Katika hatua nyingine lijualikali amesema kuwa kunafaida kubwa kwa wananchi kutumia huduma za Kibenki kwa kuhifadhi fedha pamoja na usalama wa fedha kwa wateja  na kuwaomba wananchi kuacha kuhifadhi fedha zao kwa kuzichimbia chini bali watumie fursa hiyo yakufunguliwa kwa Tawi la Benki ya CRDB Wilaya ya Nkasi kujikwamua kiuchumi.

Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Peter Lijualikali akizungumnza na wakazi wa Wilaya ya Nkasi wakati wa uzinduzi wa Benki ya CRDB Tawi la Nkasi.

Justo Ngwelo Kaimu Mkurugenzi wateja wateja wadogo Benki ya CRDB benki Makao makuu amesema kuwa Benki hiyo imekuja na fursa ya utoaji wa mikopo wezeshi kwa  Miradi bunifu  kwa vijana na wanawake inayojulikana kama IMBEJU kwa lengo la kuwainua kiuchumi.

‘’IMBEJU hii ni fursa ya kutoa mikopo wezeshi kwa Miradi bunifu ya vijana na wanawake hasa walipo kwenye vikundi tumeshuka zaidi kwaajili ya vijana na wanawake kwa kuwa hii itakuwa na masharti nafuu ‘’amesema Ngwelo.

Amesema kuwa kufunguliwa kwa Tawi la Benki ya CRDB Wilaya ya Nkasi itawasadia wananchi katika kupata mikopo pamoja na huduma za kifedha kwa wananchi kwa urahisi zaidi.

‘’huu ni wakati mwafaka kwa vijana na wanawake wa Nkasi  na jamii nzima kwa ujumla kuungana na wenzao kutoka kila kona ya nchi kujenga uchumi imara kuanzia ngazi ya mtu binafsi familia mpaka jamii kama unataka mafanikio hakikisha unahudumiwa na Benki ya CRDB’’

Joshua Mgaya Mkazi wa Wilaya ya Nkasi amesema kuwa ujio wa Benki ya CRDB utakwenda kuwa mkoambozi kwao kwa kuwa na fursa ya kupata huduma za kifedha na kupatiwa mikopo kwa kadri ya mahitaji yao.

Kauli hiyo inaungwa na Jesca Lwiza mkazi wa Nkasi ambae ameelezakuwa wananchi wa Nkasi sasa wataepukana na adha ya kufata huduma hiyo Sumbawanga kwakuwa Benki hiyo imewafikia wananchi

kufunguliwa kwa Tawi la Benki ya CRDB Wilaya ya Nkasi inafanya kufikisha Jumla ya Matawi 252 nchi nzima huku Mkoa wa Rukwa ukiwa na Mawakala 200 wanaotoa huduma za CRDB wakala ambapo kwa wilaya ya Nkasi kuna Mawakala 29.

kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa 

kataviclub.blogspot.com

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages