Wafanya biashara wa Mazao katika soko la Mahindi Mpanda hotel wakiwa katika shughuli zao za kila siku sokoni hapo |
Na Paul Mathias
Katavi.
Wafanya biasahara wa Mazao
katika mkoa wa Katavi wamesema hatua ya Serikali ya mkoa wa katavi kupiga
Marufuku wafanyabiashara kutoka nje ya nchi kwenda kununua Mazao vijijini
itapunguza mfumko wa bei ya mazao.
shuhguli za kila siku za wafanyabiashara wa Mahindi Mpanda hotel Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi |
Wafanya biasahara wa Mazao katika mkoa wa Katavi wamesema hatua ya Serikali ya mkoa wa katavi kupiga Marufuku wafanyabiashara kutoka Nje ya nchi kwenda kununua Mazao vijijini itapunguza mfumko wa bei ya mazao.
Wafanya biashahara hao wamesema
kuwa Kitendo cha serikali ya mkoa wa
Katavi kupiga marufuku wafanyabiashara kutoka nje ya nchi kwenda mojakwamoja
vijijini kununua mazao itasaidia kupunguza ongezeko la bei mara dufu kwa mazao
hususani Mpunga na mahindi.
Antony Chula mfanya biashara wa
Mahindi katika soko la Mpanda hotel Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi amesema
wafanyabiashara wa kigeni wakienda kijijini wamekuwa wakijali kujaza mzigo na
kuondoka bila kujali kuwa wanaathiri watumiaji wa bidhaa hiyo kwa kupandisha
bei hiyo ya mazao.
Moja ya mfanyabishara wa Mahindi katika soko la Mpanda hotel akizungumnza na chombo hiki kuhusu mwenendo wa biashara ya mahindi sokoni hapo |
‘’Ilikuwa ni changamoto sana kwa mfanyabiashara kutoka nje kupitiliza moja kwa moja kijijini imetuathiri pakubwa kwa maana mfano bei ya gunia la mahindi kwa hapa mjini kwa kule kijijini mfano tunanunua elfu Tisini mfanya biashara akifike kule kijijini anapandisha bei moja kwa moja’’ amesema Chula
Amempongeza mkuu wa mkoa wa
Katavi Mwanamvua mrindoko kwa hatua hiyo ya kupiga marufuku wafanya biashara wa
kigeni kwenda vijijini moja kwa moja
kununua mazao na badala yake wafanyabiashara hao wa Kigeni wanunulie Mahindi hayo Sokoni na itakuwa na tija kwa uchumi wa Mkoa wa Katavi.
‘’mkuu wa mkoa tunampongeza kwa
hayo maono ni wakuuwa mikoa wachache ambao wanaliangalia suala hilo la kutujali
sisi wafanya biashara wa ndani katika mkoa wetu’’ amesema Antony
Khadija Rashid mfanya biashara
wa wa Mahindi katika soko la Mpanda hotel wakati akizungumnza na chombo hiki
amesema hatua ya serikali ya Mkoa wa Katavi kuchukua maamuzi hayo yatakwenda
kuwanufaisha wafanyabiashara na serikali kupata mapato kwakuwa wafanya
biashara hao watakuwa wananunulia mazao hayo kutoka sokoni hapo.
‘’Wafanya biashara wanaotoka
Kenya waje kununulia mahandi haya sikoni sio kwenda moja kwa moja kwenda huko
kijijini tunaishuru serikali kwa kuliona hilo’’ amesema Khadija
‘’kwa maoni yangu mimi mkuu wa
mkoa yupo sawa hata sisi lilikuwa linatupa utata sana maana tulikuwa hatupati
faida kutokana na mfumko huo wa bei unaletwa na hao wafanya biashara wa kigeni’’
Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa
Katavi Mwanamvua mrindoko alikutana na wafanyabishara wa mkoa wa Katavi alipiga
Marufuku wafanyabiashara wa kigeni kwenda kununua mazao vijijini moja kwa moja
badala yake wafanya biashara wa mkoa wa Katavi wanunue mahindi hayo vijijini na
kuyaleta sokoni ili wafanya baishara wa kigeni wanunulie mazao hayo sokoni.
‘’wafanyabiashara wanaotoka nje
ya nchi hawaluhusiwi kununua mazao moja kwa moja shambani au moja kwa moja kwa
wakulima badala yake wafanya biashara wetu ndani ya mkoa changamkieni fursa
hiyo ya kununua mazao hayo vijijini na kuwauzia wafanyabiashara wa kigeni
sokoni ‘’amesema Mrindoko
kwa habari zaidi Tembelea ukurasa wetu wa
kataviclub.blogspot.com