Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Jamila Yusuph ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda akiwahutubia wajumbe wa Jukwaa la Maendeleo ya ushirika Mkoa wa Katavi. |
Serikali
katika Mkoa wa Katavi imeviagiza vyama vya ushirika kuhakikisha wakulima wa
Mazao ya Pamba na Tumbaku na mazao mengine yaliyo chini ya ushirika kuhakikisha
wakulima wanalipwa fedha zao pindi wanapopeleka mazao hayo sokoni.
Peter nyakunga kaimu Mlajisi Msaidizi mkoa wa katavi akitoa taarifa ya maendeleo ya ushirika kwa wajumbe wa Jukwaa la Maendeleo na Ushirika mkoa wa katavi
Serikali katika Mkoa wa Katavi imeviagiza vyama vya ushirika kuhakikisha wakulima wa Mazao ya Pamba na Tumbaku na mazao mengine yaliyo chini ya ushirika kuhakikisha wakulima wanalipwa fedha zao pindi wanapopeleka mazao hayo sokoni.
Kauli
hiyo imetolewa na Mwakilishi wa Mkoa wa Katavi Jamila Yusuph ambae ni Mkuu wa
Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi.
Akiwa
hutubia wadau wa Jukwaa la maendeleo ya ushirika katika mkoa wa Katavi Katika
ukumbi wa mikutano wa Mpanda Social Hall Jamila amesema vyama vya ushirika niwajibu
wao kuhakikisha wakulima wanalipwa fedha zao kwa wakati ili waweze kujiletea
maendeleo kupitia fedha hizo.
Amewataka
viongozi wa vyama vya ushrika kufanya kazi kwa bidii kwa kutanguliza weledi
uaminifu na uadirifu katika kazi za kila za kuvisimamia vyama vya ushirika.
Jamila
anasema ‘’nitoe rai kwa viongozi wa vyama vya ushirika na wakulima mliopo hapa
kufanya kazi kwa bidii weledi uaminifu na uadilifu katika utendaji kazi ‘’
Amsema
kuwa ushirika ni Mhimili mhimu katika sekta ya uchumi kwa kuchangia vikubwa
katika Mapato kwenye halmashauri na mkoa wa Katavi kwa ujumla.
Kaimu
Mlajisi Msaidizi Mkoa wa Katavi Peter Nyakunga amesema kuwa mkoa wa Katavi
unavyama vya ushirika vipatavyo 50 ambavyo hufanya shughuli mbalimbali ikiwemo
kilimo,Ufugaji na Saccos.
‘’katika
vyama hivyo Hamsini vya ushirika tunavyama tunavyama Arobaini na Moja vya mazao
,vyama vitano vya kifedha,vyama viwili vya ufugaji,chama kimoja cha uvuvi na
chama kikiuu kimoja’’ amesema Nyakunga
Amebainisha
kuwa Jukumu kubwa ushirika ni kusimamia utekelezaji wa sheria za ushirika na
kutoa elimu kwa wanaushirika kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu ushirika na
kutatua migogoro ndani ya vyama vya ushirika.
Amos
Kaega Mwenyekiti wa Jukwaa la Maendeleo na ushirika mkoa wa Katavi ameishuru
serikali ya awamu ya Sita kwa kuendelea bkuboresha mazingira ya sekta ya kilimo
hapa nachini na kufanya sekta hiyo kuwa mhimu katika ukuaji wa uchumi.
Mkutano
huo wa wa Jukwaa la Maendeleo ya
ushirika mkoa wa Katavi umeenda sambamba na kaulimbiu inayosema ‘’USHIRIKA KWA MAENDELEO ENDELEVU’’ KAZI
IENDELEE.
Kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa
kataviclub.blogspot.com