Na Walter Mguluchuma
Katavi,
Maafisa Tarafa na Watendaji wote wa Kata wa Mkoa wa Katavi
wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa utendaji wao wa kazi wa kila
siku na kukumbushwa mahusiano yao baina ya Serikali kuu na Serikali
za Mitaa ili kuhakikisha utawala Bora unafanyika .
Maafisa Tarafa na Watendaji wote wa Kata wa Mkoa wa Katavi wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa utendaji wao wa kazi wa kila siku na kukumbushwa mahusiano yao baina ya Serikali kuu na Serikali za Mitaa ili kuhakikisha utawala Bora unafanyika .Maafisa Tarafa na watendaji wa Kata Mkoa wa Katavi wakiwa wakisiliza uwasilishwaji wa Mada mbalimbali katika semina ya kuwajengea uwezo katika kazi zao.
Mafunzo hayo hayo yaliondaliwa na TAMISEMI
yamefunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamira Yusuph aliyemwakilisha Mkuu wa
Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo yaliofanyika
katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda .
Katika hotuba yake hiyo ya ufunguzi Jamila
Yusuph amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa viongozi hao wa
Tarafa na Kata kwani yatawaongezea uwezo wa utendaji wao wa kazi zao za
kila siku kwani uzowefu umeonyesha umeonyesha uwepo wa
uchangamoto zinazokuwepo za utekelezaji wa
huduma kwa wananchi katika ngazi ya Kata na Tarafa na
Halmashauri zinazotokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutozingatia
sheria na kanunu katika utekelezaji wa kazi za kila siku .
Kutokuwa na uwelewa kwa sheria sera na miongozo
wanayotakiwa kuisimamia na kuitekeleza ,kukosa ubunifu wa
kiongozi katika kujua furusa za kiuchumi na kijamii
zinazopatikana kwenye ngazi ya msingi pamoja na ushirikishwaji wa wananchi
na wadau kulingana na rasilamali zinazokuwepo .
Jamila amesema kuwa ni matumaini na matarajio
ya TAMISEMI ya baada ya mafunzo hayo maafisa hao wa
ngazi ya Tarafa na Kata watakwenda kutatua kelo za wananchi na
watazingatia sheria za utumishi wa umma na kutotowa siri za Serikali .
Ummy Wayayu Mkurugenzi Msaidizi
idara ya Serikali za Mitaa fedha kutoka TAMISEMI
ameeleza kuwa mafunzo hayo kwa maafisa wa ngazi hiyo yatafanyika
kwa mikoa yote na yalizinduliwa huko Mkoani
Songwe .
Amebainisha kuwa Tamisemi wameona umuhimu wa
kuwapatia mafunzo hayo maafisa hao kwa kuwa wao ndio viunganishi
baina ya Serikali kuu na Serikali za Mitaa na pia kuwakumbusha wao ndio
mzizi wa utendaji kazi kuanzia huko chini ambao wanatakiwa kutatua changamoto
zinazokuwa zimetokea kwa wananchi na kuzitatua kwenye maeneo yao .
Kwa upande wake Naibu Mkuu wa cguo cha
Serikali za Mitaa Dr Michael
Msendekwa ameeleza kuwa anaimani kuwa baada ya mafunzo
hayo watabadilika katika utendaji wao wa kazi za kila siku na yatasaidia
si kwa Katavi tuu mbali kwa nchi nzima .
Wanaamini kuwa wao maafisa hao wa ngazi ya Tarafa na
Kata wako karibu na wananchi katika kazi
zao za kila siku hivyo watahakikisha utawala bora unafanyika na
kazi za serikali zinatekelezwa .
Mmmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Afisa
Tarafa wa Tarafa ya Kabungu Alson Uisso amesema kuwa
mafunzo hayo yatawasaidia sana kuwakumbusha majukumu yao ya utendaji wao
wa kazi na baada ya hapo wataenda kuwa viongozi bora zaidi
kwenye maeneo yao ya kazi .
kwa habari zaidi tembelea ukkurasa wetu wa
kataviclub.blogspot.com