Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi akiuliza swali kuhusu ujenzi wa Mradi wa kilimo cha umwagiliaji cha Mwamkulu kilichopo ndani ya jimbo la Mpanda mjini |
Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imesema kuwa katika Mwaka mpya wa fedha na huu unaoendelea itakwenda kujenga Miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji zaidi ya 42 ukiwemo Mradi wa Kilimo cha Umwahgiliaji cha Mwamkulu kilichopo Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.
Hayo yamebainishwa na
Naibu waziri wa Kilimo Antony Bungeni Mjini Dodoma wakati wa Kipindi Cha Maswali
na Majibu kufuatia Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi alietaka
kufahamu lini utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa kilimo wa kilimo cha
Umwagiliaji wa Mwamkulu utaanza kutekelezwa.
Kapufi alitaka kufahamu
lini ujenzi huo utaanza kwakuwa utakwenda kuwa miongoni mwa miradi mikubwa
inayofanya kilimo cha umwagiliaji katika mkoa wa Katavi ndani ya jimbo la Mpanda
mjini .
Amesesema ‘’je nilini
ujenzi wa mradi wa kilimo cha umwagiliji wa Mwamkulu utaanza amehoji mbunge
huyo wa Mpanda ‘’Mjini Sebastiani Kapufi
Akijibu swali hilo Naibu
waziri wa kilimo Antony Mavunde amesema serikali katika mwaka huu wa fedha na
mwaka ujao serikali inakwenda kujenga Miradi 42 ya kilimo nchini ikiwemo ujenzi
wa Mradi wa kilimo cha umwagiliaji cha Mwamkulu.
Naibu waziri Mavunde
anasema ‘’Mh Spika napenda kujibu swali la Mh Mbunge kama ifuatavyo Mh Spika
katika Miradi 42 ya kilimo cha umwagiliaji ambazo zitaenda kujengwa katika
mwaka huu wa fedha unaoishia na ambao unaendelea ni pamoja na ujenzi wa Mradi
wa umwagiliaji wa Mwamkulu hivyo nimtoe wasiwasi Mh Kapufi ‘’amesema Mavunde
Kujengwa kwa mradi huo wa
kilimo cha Umwagiliaji mwamkulu yiatakuwa nimapinduzi makubwa ya kilimo katika
mkoa wa Katavi kwani utakwenda kuongeza mara dufu uzalishaji wa kilimo cha
Mpunga kwa wakulima wa Manispaa ya Mpanda na mkoa wa Katavi kwa ujumla.
kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa
kataviclub.blogsot.com