Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani akitoa taarifa ya Matukio mbalimbali kwa waandishi wa habari ofisini kwake. |
Na Walter Mguluchuma,Katavi.
Watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kwa kutuhuma za kumteka mtoto mdogo wa kike (9) mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya Msingi Mizengo Pinda katika Manispaa ya Mpanda na kisha kumfungia ndani ya chumba kwa zaidi ya siku moja na kutishia kumuua kwa madai vinginevyo walipwe Milioni 50 ili wamwachie .
Watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kwa kutuhuma za kumteka mtoto mdogo wa kike (9) mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya Msingi Mizengo Pinda katika Manispaa ya Mpanda na kisha kumfungia ndani ya chumba kwa zaidi ya siku moja na kutishia kumuua kwa madai vinginevyo walipwe Milioni 50 ili wamwachie .
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi
Kaster Ngonyani amewataja watuhumiwa hao walikamatwa kuhusika na
tukio hili kuwa ni Joseph John(24) Yusuph Sadick (27) wakazi
wa Mtaa wa Milupwa , Abrahamu Kassim(28) Mkazi wa Mtaa wa
Misunkumilo Manispaa ya Mpanda na Samwel Nzobe (41) Mkazi wa Mtaa
wa Kotasi Manispaa ya Mpanda .
Amesema watuhumiwa hao wote wanne wamekamatwa
kufuatia msako mkali ulifanywa na jeshi la Polisi usiku na mchana
kufatilia jeshi hilo la polisi kuwa limepata taatifa ya kutekwa kwa mtoto huyo
mdogo wa kike .
Kaimu Kamanda wa Polisi Ngonyani amebainisha kuwa
tukio hilo la kikatili la kumteka mtoto huyo lilitokea hapo June 13
majira ya saa nane mchana katika Manispaa ya Mpanda wakati mtoto
huyo alipokuwa akitokea shuleni kwenye shule anayosoma ya Mizengo
Pinda alikukuwa amekwenda kufanya usafi shule .
Ameeleza kuwa wakati akiwa njia maeneo ya jirani na Kanisa
Katoliki Jimbo la Mpanda anaelekea nyumbani kwao ndipo watuhumiwa
hao wanne walipomteka mtoto huyo na kumpeleka kusiko julikana
na kumtishia kumuua lasivyo walipwe
na mzazi wake kiasi cha shilingi milioni 50 ndipo waweze kumwachia akiwa
hai .
Baada ya taarifa hizo kuwa zimepokelewa Jeshi
la Polisi lilianza mara moja kufanya msako mkali wa kuwasaka wahusika wa
tukio hilo msako ambao ulifanyika usiku na mchana katika
maeneo yote ya Mkoa wa Katavi ili kuwahakikisha mtoto huyo anapatikana akiwa
salama .
Ngonyani amesema ndipo mnamo tarehe 14 june
jeshi la polisi walifanikiwa kumpata mtoto huyo akiwa
salama huko katika maeneo ya Mtaa wa Milupwa Manispaa ya
Mpanda akiwa amefichwa ndani ndani ya chumba cha
mtuhumiwa Joseph John.
Amesema watuhumiwa wote wanaendelea
kushikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi juu
ya tukio hili na mara baada ya upelelezi kukamilika
watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazo wakabili.