Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mpanda ikiwa katika Ziara ya kukagua Majengo ya Madarasa yanayotekelezwa kupitia Mradi wa Boost.
Na Paul Mathias,Mpanda.
Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mpanda kimeridhishwa na Mwenenendo wa ujenzi wa Vyumba vya Madarasa kwenye shule za Msingi wilaya ya Mpanda yanayojengwa kupitia Mradi wa Boost.
Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mpanda kimeridhishwa na Mwenenendo wa ujenzi wa Vyumba vya Madarasa kwenye shule za Msingi wilaya ya Mpanda yanayojengwa kupitia Mradi wa Boost.
Kamati ya siasa ya Wilaya ya
Mpanda ikiongozwa na Katibu wa chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mpanda Sadiki
Kibwana Kadulo amesema mwenendo wa miradi hiyo itakwenda kuwa saidia wanafunzi
kuyatumia Madarasa hayo pindi shule zitakapofunguliwa Mwezi wa Saba mwakaa huu.
‘’maagizo na maelekezo sisi
chama cha Mapinduzi kuhakikisha ifikapo July Madarasa haya yawe yamekamilika na
wanafunzi wawe wameingia kwenye Madarasa haya tunaamini kwamba kwa kasi hii
watoto watayatumia madarasa haya mwezi wa Saba’’ amesema Kadulo
Mkurugenzi mtendaji wa
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Sophia Kumbuli amesema halmashauri hiyo
imepatiwa fedha kiasi cha Shilingi Bilion 1.9 kwaajili ya ujenzi wa Madarasa kupitia
Mpango huo wa Boost.
‘’kwa halmashauri ya Manispaa
ya Mpanda sisi tulipokea kiasi cha shilingi Bilion 1.9 ambayo kwa pamoja
inaendelea kujenga miundo mbinu ya madarasa ambayo ipo katika hatua
mbalimbali’’ amesema Kumbuli
‘’katika fedha hizi ninashule
mbili mpya zinazojegwa ambavyo ni jumla ya Nyumba 16 ambapo vyumba 14 kwaajili
ya Wanafunzi wa Kawaida na na vyumba
Viwili kwaajili ya Madarasa ya awali ya mfano ujenzi unaendelea upo katika
hatua ya kupaua’’
Katika ziara hiyo ya kukagua miradi ya Elimu Msingi kupitia Miradi ya Boost chama cha Mapinduzi wilaya ya Mpanda kiweza kutembelea Shule ya Msingi Makanyagio,Shule ya Msingi Shanwe,Shule ya Msingi Itenka na shule ya Msingi Tumaini zilizopo halmashauri ya Nsimbo.