CCM: KATAVI YAFUNGA KAMPENI KWA KISHINDO

Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Katavi Iddy Kimanta akiwa katika kufunga za uchaguzi Mdogo wa Udiwani Kata ya Mbede Halmashauri ya Mpibwe Wilaya ya Mlele

Na Paul Mathias,Katavi

Chama Cha mapinduzi CCM katika mkoa wa Katavi kimesema kuwa hakita dharau uchaguzi wa aina yeyote utakao jitokeza katika mkoa wa Katavi.

Mgombea udiwani Kata ya Mbede Vircent Mauga akiwa amenyanuliwa juu na wanachama wa chama cha Mapinduzi baada ya kufungwa kwa Kampeni hizo jana.

Chama Cha mapinduzi CCM katika mkoa wa Katavi kimesema kuwa hakita dharau uchaguzi wa aina yeyote utakao jitokeza katika mkoa wa Katavi.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Katavi Iddy Kimanta wakati Akifunga kampeni za uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika kata ya Mbede Halmashauri ya Mpibwe Wilaya ya Mlele Mkoa wa katavi.

‘’ndugu Wana CCM wenzangu hakuna uchaguzi Mdogo Wala mkubwa uchaguzi ni uchaguzi amesisiza Kimanta’’

Amewaomba wananchi wa kata ya Mbede kujitokeza Kwa wingi katika uchaguzi huo kesho na kumchagua mgobea wa CCM ndugu vicent Mauga aliye pewa baraka zote na chama hicho kuwa Mgombea Kupitia CCM

Kampeni hizo zimehudhuriwa na Viongozi Mbalimbali wa Chama na serikali ya Mkoa wa Katavi wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Iddy Kimanta pamoja na baadhi ya Wabunge wa Mkoa wa Katavi

Kwa upande wake Mgombea wa chama hicho vicent Mauga amewaomba wananchi wa kata Hiyo kumchagua kuwa Diwani wa kata Hiyo

Jumla ya Kata 13 Tanzania Bara zinafanya uchaguzi wa Madiwani huku wapiga kura wapatao 74,642 nchinzima wanatalajia kushiriki uchaguzi huo

Uchaguzi huowa udiwani katika Kata ya Mbede  unafanyika 13/7/2023 katika kata Hiyo kufuatia kifo Cha aliyekuwa Diwani wa kata Hiyo Japhet Kabogo Kufriki Dunia.

 kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa

 kataviclub.blogspot.com

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages