MBUNGE MARTHA KUANZA ZIARA WILAYA YA MPANDA

 


Na Paul Mathias,Katavi

Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Katavi Martha Mariki anatalajia kuanza ziara yake leo 13/7/2023 kwa kutembelea Wilaya ya Mpanda ikiwa ni sehemu ya zaiara yake ya kutembelea Kata zote za Mkoa wa Katavi.


Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Katavi Martha Mariki anatalajia kuanza ziara yake leo 13/7/2023 kwa kutembelea Wilaya ya Mpanda ikiwa ni sehemu ya zaiara yake ya kutembelea Kata zote za Mkoa wa Katavi

Ziara hiyo inafuatia baada ya kukamilisha kuiitembelea Wilaya ya Tanganyika ambapo ameweza kutembelea Jumla ya Kata 15 huku akijionea namna serikali inavyo tekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa wananchi.

Akiwa katika ziara Wilaya ya Tanganyika ameweza kuwawwezesha akina mama wa UWT Ngazi ya Kata kwa kuwawezesha kiasi cha Shilingi Laki Tano Kila Kata kwa lengo la kuwainua kiuchumi kupitia uanzishaji wa Miradi mbalimbali ili kuisaidia jumuiya hiyo ya wanawake kujiinua kiuchumi.

Katika hatua nyingine ameweza kutoa Kadi 2000 za chama cha Mapinduzi kwa akinana mama wa UWT Mkoa wa Katavi kwa lengo la kuendelea kuongeza wanachama kupitia jumuiya hiyo.

Akiwa katika katika Kata ya Ilangu Mbunge Martha Mariki ameweza kuchangia Shilingi Milioni Moja kwaajili ya kuunga Mkono juhudi za wananchi wa Kata ya Ilangu halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kwa kuguswa kujitolea ufyatuaji wa tofali kwaajili ya ujenzi wa Kituo hicho.

Baadhi ya miradi aliyoitembelea akiwa katika Wilaya ya Tanganyika ni pamoja na Bandari ya Karema ambayo imejegwa na serikali ya awamu ya Sita ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan.

Mbunge huyo wa Viti maalumu Martha Mariki amewahamasisha wanawake katika wilaya ya Tanganyika kushiriki ipasavyo katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kupitia chama cha Mapinduzi.

Zaiara hiyo inaanza leo katika Wilaya ya Mpanda kwa kuzitembelea Kata za Mpanda hotel na Kata ya Majengo zilizopo halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ikiwa ni sehemu yake ya kutembelea Kata zote 58 zilizopo mkoa wa Katavi.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages