DC MPANDA AISHAURI JAMII KUTUMIA MIUONDOMBINU ILIJENGWA YA ELIMU KWA MANUFAA YA NCHI


Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Jamila Yusuph akizungumza na kamati ya ushauri ya wilaya ambapo ameiomba jamii kutumia miundombinu ya elimu iliyojengwa kwa ajili kwa manufaa ya nchi (Picha na George Mwigulu)

Na Walter Mguluchuma,Mpanda.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  Jamila  Yusuph  amewataka wananchi wa   Wilaya hiyo  kuhamasisha jamii kupeleka  watoto shule kwani  kwa sasa   miundombini ipo ya kutosha ya madarasa ya shule za msingi na Sekondari  na vyuo kwa wanaomaliza kidato cha nne na darasa la saba vipo  hivyo wawasimamie watoto  waweze kwenda shule miundombinu hiyo itumuke kwa watoto wa wana  Mpanda  mwisho wa siku  wawe wapate kuwa viongozi wanchi  hii na kuwaongoza watu wengine wa nchii hii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Mpanda,Sophia Kumbuli akizungumza jambo na Katibu Tawala wa Wilaya ya Mpanda  Mwashitete( Picha na George Mwigulu)

Wito huo ameutowa  wakati wa kikao  cha wadau wa  maendeleo  wa Wilaya ya Mpanda kilichofanyika katika ukumbi  wa Manispaa ya Mpanda kwa ajiri ya kujadili  maswala ya  maendeleo  ya   Wilaya hiyo .

Aliwasisitiza wajumbe wa kikao hicho kuwa  mabalozi  wa kuwahasisha jamii kupeleka watoto shule  kwani Serikali imeisha weka miundombinu ya kutosha kwenye shule za msingi na Sekondari  na pia kwenye Wilaya ya Mpanda vipo vyuo mbalimbali kama vile chuo cha afya, Veta na  chuo cha Wananchi Msaginya  .

Amebainisha kuwa kwenye vyuo hivyo wanaweza kwenda watoto waliomaliza elimu ya kidato cha nne na pia waliomaliza  darasa la saba wanaweza  kwenda  kwenye chuo cha wananchi Msaginya na veta Mpanda .

Dc  Jamila  aliwataka  kutumia  vizuri miundombinu hiyo vizuri  kwa manufaa ya watu wa Mpanda  ili na  wao  watoto mwisho wa siku waweze na wao kuwa viongozi katika  nchi hii na kuweza kuwaongoza wengine  hivyo miundombinu hiyo iliyojengwa isibaki bila watoto kwenda kuitumia .

Amewaomba wananchi wananchi kuhakikisha  miundombinu  yote  inayoletwa katika Wilaya ya Mpanda   kama vile ya elimu   maji  barabarana mingineyo kuhakikisha wanaitunza  vizuri ili iwezekudumu muda mrefu zaidi   kwa manufaa ya sasa na hapo baadae .

Swala jingine amewaomba wadau wa maendeleo kusimama kwa  pamoja  kuupinga  ukatili wa aina yoyote ile      pamoja na kukataa  mmonyoko wa maadili kama  vitendo vya ubakaji ,usagaji  vitendo vya ushoga mimba za utotoni   wote wasimamame kwa pamoja na Mungu atawabaliki kwa kupinga vitendo hivyo .

Alisema kwa sasa watoto wamekosa  malezi mazuri   hali ambayo imesababisha kuwa wanafanyiwa vitendo vya ukatili  sana  hasa watoto wa kiume na wamakuwa wakifanyiwa na wengine ndugu zao  wa karibu hata wakuzaliwa  anachokizungumza wameisha kifanyia uchunguzi  wamebaini hayo.

Wajumbe wakiwa kwenye mkutano leo katika ukumbi wa manispaa ya Mpanda (Picha na George Mwigulu)

Jamila alisema   ni vema  kuwa watu wanafanya mazungumzo na watoto wao  wasiseme tuu wapo  na    ndugu zao wanalala pamoja wawe na utaratibu wa kuzungumza nao  na ikibidi  kuwakagua kwasababu watoto  wetu wanaumizwa sana na walezi  kwa sababu wazazi tumekuwa tujishughulisha sana na mambo mengine na kusahau kuwaangalia watoto.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Sofia Kumbuli amesema kuwa Rais  Dkta Samia  Suluhu sana  amesema  Manispaa ya Mpanda wametendewa haki sana kwa kuboreshewa Hospitali ya  Manispaa ya Mpanda  ambapo ukifika   pale kwa sasa ni kama vile umefika kwenye Hospitali ya kubwa  za Rufaa  kwa jinsi ilivyokarabatiwa na   inavyoendelea kujengwa .

Amesema katika kuunga jitihada   hizo za  Rais  samia  Manispaa hiyo  inatajia kujenga  madarasa ya shule za msingi mia moja ili  kwa kupitia frdha za mapato ya ndani ya Halmashari hiyo ili kuondoa tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa .

Mzee  maarufu wa Mji wa Mpanda Vicent Nkana alisema kuwa  hali ya ulinzi na usalama katika  mkoa wa Katavi  anaiona imeimarika sana tofauti na hali ilivyokuwa katika miaka ya hapo nyuma wananchi walikuwa    hawaishi  kwa  amani.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages