SERIKALI KUJENGA SHULE YA SEKONDARI WASICHANA MASOMO YA SAYANSI KATAVI.

 

Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Katavi, Martha Mariki akizungumza na wanawake wa UWT kata ya Kapalala pamoja na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM alipotembelea Kata hiyo.

Na Paul Mathias,Nsimbo

Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki ameipongeza serikali kwa kutoa shilingi Bilioni 3 Kwaajili ya ujenzi wa Sekondari ya wasichana maalumu ya Mchepuo wa Sayansi itakayo jengwa katika Kata ya Kapalala halmashauri ya Nsimbo.

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Katavi,Martha Mariki akipokelewa kwa Shangwe na wanawake wa UWT Kata ya Nsimbo.

Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki ameipongeza serikali kwa kutoa shilingi Bilioni 3 Kwaajili ya ujenzi wa Sekondari maalumu ya wasichana ya Mchepuo wa Sayansi itakayo jengwa katika Kata ya Kapalala halmashauri ya Nsimbo.

Hayo yamebainishwa na Mbunge huyo wakati akiwa katika  Ziara katika Kata ya Kapalala   wakati akizungumza na wanawake wa UWT Katika Kata hiyo.

Amesema hatua hiyo ya serikali kuleta fedha Bilioni 3 kwaajili ya kujenga shule hiyo itasaidia wanafunzi wa kike kupenda masomo ya Sayansi na kuweza kupata watalaumu wengi wa Masomo ya Sayansi katika mkoa wa katavi.

 

Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi,Martha Mariki akiwa katika ziara katika Kata ya Nsimbo.

'’Bilioni tatu zimekuja kwaajili ya ujenzi wa shule maalumu ya Sayansi ya Wasichana hii shule ingeweza kujengwa maeneo mengine lakini kwa kuwa mnajua mama wa Jimbo hili Anna lupembe ni mama mahili ameisemea Nsimbo mpaka shule shule hii ya kimkoa kuja kujengwa hapa Kapalala’’amesema Mbunge huyo.

Katika hatua nyingine amesema serikali imeleta fedha kiasi Cha shilingi Milioni 600 kwaajili ya ujenzi wa Sekondari Kapalala hatua ambayo itaendelea kuimalisha upatikanaji wa Elimu kwenye kata.

Mbunge Martha anasema ‘’kwanza mmepewa shilingi Milioni 600 kwajili ya ujenzi wa sekondari ya Kata hizi zote ni juhudi za serikali ya kuhakikisha wananchi wa Kapalala na Nsimbo kwa ujumla huduma mhimu ikiwemo elimu inatolewa katika miundo mbinu rafiki’’

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Katavi,Martha Mariki [Katikati] akiwakabidhi  laki Tano wanawake wa UWT pamoja na vingozi wa Chama Kata ya Kapalala

Mbunge huyo akiwa katika kata ya Nsimbo halmashauri ya Nsimbo amesema hatua ya serikali kuendelea kuleta fedha katika sekta Mbalimbali ni sehemu ya serikali kuhakikisha huduma za kijamiii zinazosogewzwa karibu na Wananchi.

‘’kuna fedha nyingi sana za miradi ya zimeletwa katika kata hii ya Nsimbo kwenye kata hii tu ya Nsimbo tumeweza kuletewa na serikali zaidi ya Bilioni 1.9 na haya yote mnayoyaona yanakuja niusimamizi mzuri wa chama cha Mapinduzi’’ amesema Mb Martha Mariki.

Mbunge Huyo amewakumbusha waanchi hao kusimama katika malaezi mema Kwa Watoto wao Ili kukabiliana na tatizo la mporomoko wa maadili katika jamii ambalo limepelekea baadhi ya Watoto kujiiunga katika vikundi vya Watoto waharifu.

Wanawake wa UWT Kata ya Nsimbo wakiwa katika ishara ya kufurahia Jambo wakati Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi,Martha Mariki alipokuwa anazungmza nao mapema leo.

Mbunge Martha Mariki yupo katika ziara ya ya Kutembelea Kata za Mkoa wa Katavi na Leo ametembelea Kata ya Nsimbo na Kapalala ambapo ametoa Laki Tano Kwa Kila Kata Kwa wanawake wa UWT pamoja na Kadi za UWT ili kuendelea kuingiza wanachama wengi zaidi 

Ziara hiyo inatalajia kuendelea Katika Kata za Ibindi na Itenka hatua ambayo itafanya kumaliza Kuzitembelea Kata zote 12 zilizopo Jimbo la Nsimbo Wilaya ya Mpanda.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages