Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani. |
Na Walter Mguluchuma,Katavi.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limekanusha taarifa ambazo zimesambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii zikieleza kuwa Pambano Kamaka (40) Mkazi wa Mtaa wa Makanyagio Manispaa ya Mpanda ambae alijeruhiwa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani kuwa alifanyiziwa kitendo hicho kwa sababu za kisiasa sio za kweli na wananchi wanatakiwa wapuuze uvumi huo wa uongo.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limekanusha taarifa ambazo zimesambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii zikieleza kuwa Pambano Kamaka (40) Mkazi wa Mtaa wa Makanyagio Manispaa ya Mpanda ambae alijeruhiwa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani kuwa alifanyiziwa kitendo hicho kwa sababu za kisiasa sio za kweli na wananchi wanatakiwa wapuuze uvumi huo wa uongo.
Kamanda wa P olisi wa
Mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani amewaambia wandishi wa Habari kuwa
Pambano Kamaka ambae ni Katibu Mwenezi
wa Kata ya Makanyagio Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) alipigwa na kitu
kizito kichwani na kupoteza fahamu .
Alisema uchunguzi
uliofanywa na jeshi la Polisi baada ya kumkamata
mtuhumiwa mmoja aitwaye Gilibalt Jaluo
mkazi wa Mtaa wa Makanyagio ambae alihusika kwenye tukio la kumpiga
Kamaka umeonyesha kuwa alipigwa kutokana deni alilokuwa akidaiwa la
Tshs 50,000 na mtuhumiwa mwingine .
Kamanda
Ngonyani alisema mtuhumiwa huyo mwingine aliyekuwa akimdai
kiasi hicho cha fedha alikimbia mara baada ya kuwa
wametenda kosa hilo la kumpiga na kitu kizito kichwani
mhanga huyo.
Amesisitiza
kuwa tukio hilo halina ukweli wowote kama ambavyo
limeripotiwa na mitandao ya kijamii kuwa linahusiana na
maswala ya kiasiasa tukio hilo halihusiani na maswala
ya kiasiasa hivyo wananchi wapuuze uvumi huo wa uongo na
wanamtafuta mtu huyo aliyeeneza habari hizo za uongo
kwenye mitandao ya kijamii .
Jeshi la
polisi Mkoa wa Katavi linaendelea na msako mkali wa
kusaka mtuhumiwa huyo aliyekimbia ili waweze
kumkamata ili hatua kali za kisheria
zichukuliwe dhidi yao waliohusika kutenda kitendo hicho cha
kikatili .
Aidha Kamanda
Ngonyani amewaomba wananchi kuendelea kutowa taarifa za
uhalifu kwenye mamlaka husika na kisha
kuziachia mamlaka hizo kufanya uchunguzi ili
kubaini ukweli wa taarifa hizo na sio kusambaza
taarifa zisizo rasmi kwenye mitandao ya kijamii
na sehemu nyingine kwani zinaleta taharuki kwenye jamii
.
Hari ya
Pambano Kamaka ambae amelazwa katika Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Katavi bado haiendelei vizuri na
taratibu zinafanywa za kumpeleka katika Hospitali ya
Kanda Mbeya zinaendelea kwa ajiri ya matibabu zaidi .