FEDHA MIL 2.9 ZATOLEWA MASHINDANO YA SANAA NA MICHEZO NSIMBO.

Mbunge wa Jimbo la Nsimbo wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Anna Lupembe akizungumza na wananchi wa Kata ya Ibindi leo wakati wa bonaza la kuibua vipaji vya uibaji wanyimbo mbalimbali.


Na George Mwigulu,Nsimbo.

Zaidi ya fedha milioni mbili na laki tisa zimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Nsimbo,Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Anna Lupembe kama zawadi kwa washindi wa mashindano mbalimbali ya michenzo katika Kata ya Ibindi mkoani hapa.

Utoaji wa zawadi huo ni mwendelezo wa jambo ambalo analifanya katika ziara yake ya kikazi jimbo humo ambapo amefanya pia katika Kata ya Itenka na Tumaini hivi karibuni.

Mbunge huyo akizungumza leo katika Kata ya Ibindi wakati wa utoaji wa zawadi hizo amesema kuwa nia ya kufanya mabonaza ya michezo mbalimbali ni kuibua vipaji hasa kwa vijana ili waweze kufikia ndoto zao.

Lupembe ameeleza kuwa anafurahi kuwa karibu zaidi na wananchi wake kama familia moja ambapo muda wa michenzo huo anautumia kukaa na wananchi pamoja na kuzungumza masuala ya maendeleo ya kijimbo.

“maana ya  kuwa mbunge ni kukaa pamoja na wananchi wako kuzungumza mambo mbalimbali ya kiamendeleo kama familia hivyo kwangu nafurahia kuwa karibu na wananchi wangu tukifurahi na kutizama ngoma na michezo mbalimbali” amsema mbunge huyo.

Vilevile amesema kuwa mpango wake ni kuhakikisha vijana wanashiriki zaidi kwenye michezo kwani baada ya mashindano hayo ya muziki ya aina mbalimbali kukamilika kwa ngazi za kata na washindi kupatikana atafanya pia ya ngazi ya jimbo hilo.

Aidha katika washindi wa mpira wa miguu ngazi ya kata kupitia ligi ya Lupembe CUP wamepewa zawadi ya fedha ambapo mshidi wa kwanza Tsh 500,000/=.Mshindi wa pili Tsh 300,000/= Mshindi wa tatu Tsh 200,000/- na mshindi wan ne Tsh 50,000/= kama kifuta jasho.

Vilevile kwenye mashindano ya mziki kupitia vikundi vyao na waibaji binafisi mshindi wa kwanza kapewa fedha Tsh 300,000/= mshindi wa pili Tsh 200,000/= mshindi wa tatu Tsh 100,000/= na mshindi wan ne Tsh 50,000/=

Baadhi ya washindi mbalimbali wakikabidhiwa zawadi zao leo katika Kata ya Ibindi,Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi na Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna Lupembe.

Baadhi ya washindi Madirisha Malasa amemshukuru mbunge huyo kwa kazi nzuri ya kuinua vipaji katika kata yao ambapo amesema wataendelea kumwamini kuwa mbunge wao hata kwa miaka mingine ijayo kwani shughuri zake zimekuwa zikiwagusa moja kwa moja.

Malasa amewaomba vijana kuendelea kushiriki kwenye shughuri za Sanaa mbalimbali kama vile michezo kwa sababu ni afya na inajenga udungu kati yao.

Joyce Paul ambaye ni mdau wa ngoma za asili amesema kuwa kitendo ambacho anafanya mbunge wa Jimbo la Nsimbo,Anna Lupembe ni jema na linamasirahi mapana kwa hasa kwa vijana kwani michenzo ni ajira.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages