KAMPUNI YA MKWAWA YALALAMIKIWA KWA KUTOWALIPA WAKULIMA WA TUMBAKU KATAVI.

Hii ni picha ya siku ya uzinduziI wa makoso ya Tumbaku uliofanywa na Kampuni ya Mkwawa Leaf. Meneja wa Bodi ya Tumbaku Mkoa wa Katavii,Genwin Swai alipokuwa akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko.(Picha na Makitaba).

Na Mwandishi wetu,Katavi .

Wakulima wa   vyama   vya  AMCOS  vya  Nsimbo na Kasekese wameilalamikia  Kampuni ya   ununuzi wa Tumbaku ya Mkwawa Leaf  Tobacco Limeted kwa kukiuka  mkataba  wa ununuzi wa Tumbaku  kwa kushindwa kuwalipa  malipo yao ya  ununuzi wa Tumbaku ya msimu wa  2022/2023 na kuwasababishia wakulima kuishi kwa shida.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Mkwawa Leaf Tobbaco,Ahmed Mansoor akizungumza katika Mkoa wa Katavi  wakati wa uzinduzi wa masoko ya zao  la tumbaku (Picha Na Makitava)

Baadhi ya wakulima hao wamedai kuwa  baada ya kuingia mkataba na vyama vyao walitegemea kuwa  Kampuni hiyo ingekuwa msaada mkubwa  kwa wakulima wa zao la Tumbaku katika  Mkoa wa Katavi .

Mmoja wa wakulima wa  Amcos ya Nsimbo  Gedson Simon amesema kuwa  toka walipofanya soko la  ufunguzi   mnamo tarehe  3 Mei  2023 walipo  uza tumbaku yao kwa mara ya kwanza  hadi sasa  wakulima wa kwenye chama hicho  hawalipwa  fedha zao licha ya wao mara kwa mara kuwa wanafatilia kwenye Amcos yao wamekuwa wakijibiwa kuwa kuna shida ya Dolla.

Amebainisha kuwa  kabla ya kuanza msimu   wa ununuzi wa  Tumbaku  uongozi wa Kampuni hiyo waliwaaminisha wakulima  kwa kuwaeleza kampuni hiyo  ikisha nunua  Tumbaku watakuwa wanalipa kwa wakati jambo ambalo limekuwa tofauti .

Amebainisha kuwa kitendo cha kutolipwa kwa wakati  kimewasababishia wakulima kupa adha kubwa  kutoka kwa watu ambao walikuwa wamewaajiri kwa ajiri ya shughuli za kilimo hicho ambao wameshindwa  kuwalipa  haovibarua wao hali inayofanya waendelee kuwahudumia hadi sasa kwa chakula na matibabu pindi wanapokuwa wamepata maradhi .

Alisema  wao kama wakulima wanategema  walime tumbaku  na kuiuza ili waweze  kuhudumia familia za lakini kwa wakulima wa Nsimbo  hali imekuwa tofauti na matarajio yao hivyo wanaiomba Serikali iweze kuangalia namna ya kuwasaidia waweze kulipwa fedha zao .

Juma  Mwiga    Mkulima wa Amcos ya Kasekese  Juma  Mwiga  ameeleza kuwa wao kama wakulima wameweza kuuza tumbaku yao kwa wakati  ila malipo yao ndio yamechelewa na kila wakiwauliza viongozi wanaambiwa Dolla  zimeisha hali ambayo inawafanya wakulima kutojua watalipwa lini  kwani ni mda mrefu toka walipo uza tumbaku yao .

Wanaiomba Serikali  iwasaidie kama changamoto ni Dolla  ili walipo yao yafanyike mapema kwani kazi ya kilimo cha Tumbaku ni  kubwa sana wanachukua  muda  muda mrefu wa maandalizi ya kilimo  mpaka leo hii  fedha inapochelewa  wanashindwa wafanye nini matokeo yake wamejiingiza kuchukua mikopo ya fedha za riba hivyo hata kama   watalipwa fedha  kwa hali iliyopo sasa zitaichia kwenye kulipia madeni hayo ya liba .

Amesema anachofahamu  kwenye  Mabenki ambako vyama vyao  vya AMCOS  waliko  kopa  fedha za  pembejeo huwa fedha zikichelewa kulipwa huwa kuna liba  sasa  kwa chelewa huku ili liba  atalipa nani wakati mkulima yeye sio kosa lake .

Mwenyekiti wa Nsimbo  Amcos  Gredo Kasokola  amesema  malalamiko ya wakulima ni    haki  kwani  masoko licha ya kuanza mwezi wa  tano  na    kumaliza june 22 kwenye  chama hicho  kwa mujibu wa  mkataba wao na Kampuni ya  Mkwawa wanatakiwa kila wanapokuwa wamenunua  tumbaku wanatakiwa walipe  ndani ya siku 14.

Amebainisha kuwa hadi sasa wanadai kwenye Kampuni hiyo zaidi ya Dolla milioni moja  wamekuwa wakifanya  mawasiliano na  kampuni   hiyo juu ya madai yao  kuwa  kwa sasa hawana dolla za kuwalipa.

Amesema kuwa wakati wa  maadhimisho  ya sikuuu ya Ushirika  Waziri wa Kilimo  Hussein  Bashe alisema  swala la wakulima kutolipwa  fedha zao   Wizara inalishughulikia      na ifikapo    tarehe 30  Julai swala lilo litakuwa limeshughulikiwa.

Mrajisi  msaidizi wa  vyama vya ushirika Mkoa wa Katavi  Perer Nyakunga  amasema kuwa ni kweli vyama hivyo  hawaja lipwa fedha   fedha zao la   kampuni ya Mkwawa  licha ya masoko ya ununuzi kwa Mkoa wa  Katavi msimu wake  kuwa umemalizika pia toka  tarehe 13 julai  .

Amefafanua kuwa kwa mujibu wa mikataba ya ununuzi  na uuzaji wa tumbaku  Makampuni yanatakiwa kulipa fedha ndani ya siku   kumi  nan ne baada ya kufanya ununuzi  wa soko la tumbaku  na wakulima  huwa wanalipa kwa  mikopo ya fedha za kutoka kwenye mabenki  lakini   kwa sasa kilichokwamisha ni Kampuni hiyo kutokuwa na dolla.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages