Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Katavi Martha Mariki akizungumza na wanawake wa UWT na Wanachama wa chama Cha Mapinduzi CCM katika Kata ya Majengo na Mpanda hotel |
Na Paul Mathis,Mpanda.
Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki amesema serikali ya awamu ya Sita ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan inania ya dhati ya kuimalisha Huduma za afya kwa mkoa wa Katavi .
Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki amesema serikali ya awamu ya Sita ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan inania ya dhati ya kuimalisha Huduma za afya kwa mkoa wa Katavi .
Akizungumza na wanawake wa umoja wa Chama cha Mapinduzi CCM [UWT]Katika kata za Mpanda hotel na Kata ya Majengo zilizopo halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi.
Amesema
kuwa Kujengwa kwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Katavi pamoja na hospitali za
Wilaya katika mkoa wa Katavi unaonyesha namna serikali imedhamiria kuimalisha
huduma za afya katika mkoa wa Katavi.
Amewaomba
wanachama hao kuendelea kuiunga mkono serikali ya Rais Dk Samia Suluhu na chama
cha Mapinduzi CCM kwakuwa Chama na serikali yake chini ya Chama hicho kinania
ya dhati ya kuwatumikia watanzania kwa vitendokwa kuleta maendeleo kwa wananchi.
Amewakumbusha
wanachama hao kuendelea kuyasema mazuri yanayofanywa na serikali kwa wananchi ambao wanabeza Jitihada za serikali
katika kuwatumikia wananchi.
Katika
ziara hiyo Mbunge huyo ametoa shilimgi Laki Tano kwa umoja wa wanawake wa Chama
cha Mapinduzi CCM [UWT] katika Kata za Mpanda hotel na Majengo ili kujiinua
kiuchumi.
Mwenyekiti
wa Umoja wa wanawake UWT Wilaya ya Mpanda Tausi Ramadhani amewaomba wanawake
hao kutumia fursa hiyo kukopeshana kupitia shuguli ndogo za kiuchumi.
Diwani
wa Kata ya Majengo William Mbogo amesema kuwa anaridhishwa na kazi zinazofanywa
na wabunge wote wa mkoa wa Katavi kwa lengo la kuhakikisha mkoa wa Katavi
unapiga hatua kimaendeleo.
Ziara ya Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Katavi Martha Mariki imeanza leo katika Wilaya ya Mpanda kwa kuanza kufanya ziara katika kata zilizopo Manispaa ya Mpanda