RAMLI CHONGANISHI KIKWAZO MAPAMBANO YA UKATILI KWA WATOTO

 

Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki akizungumza na wanawake wa UWT kata ya Kawajense katika ziara ya kutembelea kata za mkoa wa Katavi

Na Paul Mathias,Mpanda.

Kukithtiri kwa vitendo vya ukatili wa Kijinsia kwa watoto katika baadhi ya jamii ya Mkoa wa Katavi inasabibwa na baadhi ya jamii kuamini Mila potofu zinazotokana na ramli chonganishi zinazochochewa na baadhi ya waganga wa jadi.

Viongozi wa UWT kata ya Kawajense wakiwa katika Picha ya Pamoja na Mbunge wa Vitimaalumu mkoa wa Katavi alipotembelea kata hiyo 

Kukithtiri kwa vitendo vya ukatili wa Kijinsia kwa watoto katika baadhi ya jamii ya Mkoa wa Katavi inasabibwa na baadhi ya jamii kuamini Mila potofu zinazotokana na ramli chonganishi zinazofanywa na baadhi ya waganga wa jadi.

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki wakati wa ziara yake ya Kutembelea  kata za mkoa wa Katavi wakati alipokuwa anazungumza na Wanawake wa UWT Kata za Kawajense na  Kazima Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi.

Amebainisha kuwa baadhi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia Kwa watoto ikiwemo Ubakaji na Ulawiti vinachangaiwa na baadhi ya watu kuamini nguvu za giza kupata mafanikio ya kimaisha Kwa kupigiwa ramli na Waganga wa Jadi Kwa Kwa kuamini kuwa kufanya hivyo watafanikisha mipango ya maisha.

"Vitendo hivi vya ukatili wa Kijinsia katika mkoa wetu wa Katavi na maeneo mengine vinatokana na baadhi ya watu kuwaamini Waganga wa Jadi ambao huwadanganya watu ukitaka kupata mafanikio nenda Kabake au kamwigilie mtoto hii ni imani potofu ndungu zangu tuaache kuamini vitendo hivi Utajiri unakuja Kwa kufanya kazi"amesema Martha

Amesema Kila mmoja nilazima awe msitari wa mbele katika kutokomeza vitendo vya Ubakaji na Ulawiti Kwa watoto na kukemea vikali baadhi ya wanaume ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya Ubakaji na Ulawiti nakusisitiza serikali itaendelea kuchukua hatua Kwa wote watakaobainika na vitendo hivyo.

"ndugu zangu akina mama wenzangu unakuta mwanaume anamwigilia mtoto wa umri mdogo Kwa Kwa imani zake zake potofu ukiangalia sisi wanawake tupo, tena ni wengi sana niwaambie tu serikali ipo macho na wote wakataobainika watafikishwa Katika vyombo vya Sheria'' Amesema Mbunge huyo

Aidha Katika kukabiliana na Tatizo la Ubakaji na Ulawiti Kwa watoto wa kike na kiume amesema Moja ya changamoto kubwa ambayo jamii imeshidwa kuwajibika ni masuala hayo ya ukatili wa Kijinsia kuyamaliza matatizo hayo kiundungu Kwa baadhi ya watuhumiwa au wahusika wa vitendo hivyo.

Martha amesema "takwimu zinaonyesha kuwa Vitendo hivi vinafanywa na watu wa Karibu yaani ndugu inapo bainika, kumekuwa na tabia Kwa baadhi ya ndungu kufanya Suluhu Kwa Kigezo cha Udungu au mjuano bila kujali madhara ambayo watoto huyapata kisaikolijia baada ya kufanyiwa vitendo hivyo"

Diwani wa Kata ya Kazima Linus Tundila pamoja na Diwani Kata ya Kawajense Uwezo Bacho  Kwa pamoja wameishkuru serikali ya Awamu ya Sita namna ambavyo imekuwa ikileta fedha mbalimbali za maendeleo katika sekta ya Afya,Elimu,Barabara,na uwezeshaji wa wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu kupitia Mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na Halmashauri kwenye Kata zao.

Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki Katika kutambua mchango wa UWT kiuchumi Katika Kata ya Kawajense na Kazima ametoa shilingi Laki Tano Kwa Kila Kata  Ili kuendelea kuongeza wanachama wa Jumuiya Hiyo.

Ziara ya Mbunge huyo sasa inapiga hodi Katika Jimbo la Nsimbo baada kutamatika katika Jimbo la Mpanda Mjini kwa kuzitembelea Kata 15 za Manispaa ya Mpanda.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages