WASTAAFU WATARAJIWA WAJENGEWA UWEZO NAMNA YA KUISHINJE YA MFUMO

 

Wastaafu Watarajiwa wakipata maelezo ya kutumia fursa zilizomo ndani ya benki ya Posta baada ya kustaafu
Na Israel Mwaisaka,Rukwa

Benki ya Posta (TCB) mkoani Rukwa imewajengea uwezo Wastaafu na wanaotarajia kustaafu namna njema ya kuishi baada ya kustaafu ikiwa ni pamoja na matumizi sahihi ya kiinua mgongo.

Akizungumza na Wastaafu wilayani Nkasi meneja mkopo wa benki ya Posta makao makuu Roda Yaledi amesema kuwa benki hiyo imejipanga kuhakikisha inawasaidia Wazee hasa eneo la fedha ikiwemo na kuwapatia mikopo.

Amesema kuwa lengo mahususi la benki hiyo ni kuwawezesha wastaafu kupata kiasi kikubwa cha fedha kulingana na viwango vya malipo  ya pensheni zao za kila mwezi.

Amedai kuwa wao kama benki kwa kuthamini Wazee imejikita katika kuwawezesha wastaafu kukidhi mahitaji halisi ya fedha na kuboresha zaidi maisha yao ili kukidhi gharama za matibabu na kulipa ada za shule.

Pia amewataka Wale wanaotarajia kustaafu kuendelea kufanya maandalizi ya kustaafu ya kuishi nje ya mfumo waliouzoea ili kuendana na maisha mapya na kutoathirika kisaikolojia na kuishi sawa na wenzao.

Meneja wa TCB (Tanzania Comercial Bank) mkoa Rukwa Dismas aliwaambia Wastaafu kwamba benki yao inawatambua na wameweka utaratibu mzuri wa kuhamisha akaunti anayopokelea mafao kutoka katika benki yake ya awali na kwenda Benki ya Posta ambako pia wananunua na madeni ya benki anakotoka.

Alisoni Kijalo mmoja wa Wastaafu aliishukuru benki hiyo kwa kuendelea kutoa elimu za mara kwa mara kwa Wastaafu na kuwa hata mikopo waipatayo inawajengea uwezo mkubwa wa kuhimili gharama za maisha.

Alidai kuwa kitendo cha Wastaafu kupewa uwezo wa kukopa wakati wote bila ya kujali umri wao kunawafanya wapate ahueni.

Benki ya Posta Nchini imejikita katika kuwaandaa Wastaafu kwa kuwapatia mafunzo ya ujasiliamali na mikopo sambamba na kuwa na akaunti maalumu maalumu kwa Wazee na kuwa bima ya Nishike mkono ambayo ni maalumu kwa vikundi vya wastaafu.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages