Anna Lupembe,Mbunge wa Jimbo la Nsimbo wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi akiwahutubia wananchi wa kata ya Uruwila.
Na George Mwigulu,Nsimbo.
Wauguzi wa afya katika halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi wametakiwa kuzingatia maadili yao ya kazi wanapotoa huduma kwa wananchi pindi wanapokwenda katika zahanati kutafuta matibabu.
Wauguzi wa afya katika halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi wametakiwa kuzingatia maadili yao ya kazi wanapotoa huduma kwa wananchi pindi wanapokwenda katika zahanati kutafuta matibabu.
Wito
huo umetolewa leo na Mbunge wa Jimbo la Nsimbo,Anna Lupembe wakati wa ziara
yake ya kikazi katika Kata ya Uruwila ambapo amepokea malalamiko ya baadhi ya wanawake wa kata hiyo kuwa
wanachoteshwa ndoo za maji pindi pale wanapojifungua kwenye baadhi ya zahanati.
Baadhi ya wanawake wakitoa kero zao kwa mbunge huyo wameeleza kuwa wanapopata uchungu na kwenda kujifungua katika zahanati za serikali wanapomaliza kujifungua kabla hawajaruhusiwa wamekuwa wakitakiwa kuchota ndoo tano za maji wakati huo ni wazazi na hawana nguvu za kuchota maji.
Lupembe
amesema kuwa muuguzi ni kipaji ambacho wamepewa na Mungu na wanatakiwa kuwa na
huruma kwa wananchi.
Revocatus Mapula
Mtendaji wa Kata ya Uruwila amekiri kuwepo kwa vitendo hicho kwa kipindi cha
zamani lakini kwa sasa walishapiga marufuku na hakipo tena.
“nilimwita
inchaji wa zahanati hiyo nikamwambia ni marafuku mama yeyote akijifungua wewe
umwagize akachote maji…huko nyuma kweli lilikuwepo na kwa bahati nzuri kwenye
kikao cha Isagala juzi tuliliongelea na kulitolea ufafanuzi na Mh Diwani
akakemea hilo.Sasa kama linaendelea tunaomba mtuletee ili tulishughulike” Amesema Mapula.