LUPEMBE ATEMBELEA MAKANISA NA KUTOA MILIONI MOJA NA LAKI TANO

 

Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna Lupembe akizungumza na waumini wa kaisa Katoliki Kigango cha Stalike Parokia ya Ilembo ambapo ametoa shilingi Laki tano kwa wanakawaya kwaajili ya kusaidia ununuzi wa Kinanda 

Na Alex Ngereza,Nsimbo

Kanisa la Pentekoste Motomoto Kijiji cha Kaburonge Kata ya Katumba Jimbo la Nsimbo Mkoa wa Katavi limememshukuru Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna Lupembe kwa kuwachangia kiasi cha Shilingi Milioni Moja kwaajili ya Maendeleo ya Kanisa hilo.

Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna Lupembe [kulia] akikabidhi shilingi Milioni Moja kwa Mchungaji kiongozi wa Kanisa hilo Beteria Beny

Kanisa la Pentekoste Motomoto Kijiji cha Kaburonge Kata ya Katumba Jimbo la Nsimbo Mkoa wa Katavi limememshukuru Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna Lupembe kwa kuwachangia kiasi cha Shilingi Milioni Moja kwaajili ya Maendeleo ya Kanisa hilo.

Pongezi hizo zimetolewa na Mchungaji kiongozi wa Kanisa hilo Beteria Beny wakati wa ibaada ya jumapili iliyofanyika Kanisani hapo amesema kuwa wanamshukuru Mbunge huyo kwa kuwasaidia kiwango hicho cha fedha kwani zitawasidia katika maendeleo ya kanisa.

Mchungaji huyo amewaomba viongozi mbalimbali kuwa na moyo wa kusaidia jamii ikiwemo makanisa kama hazina ya kujiwekea mbinguni kupitia sadaka wanazo zitoa kwenye Jamii.

Akikabidhi Fedha Hizo Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna Lupembe amesema kuwa aliahidi kutoa fedha hizo wakati wa ziara yake alipofika katika kanisa hilo ili kuwasaidia katika maendeleo ya kanisa .

Aidha ametoa rai kwa wazazi na walezi kutumia fursa ya miundombinu ya serikali hususani elimu kuwapeleka watoto wao shule ili kuwa na Taifa lenye maarifa na ujuzi kupitia elimu.

Wakati huo mbunge Anna Lupembe akiwa katika ibaada ya Misa ya Jumapili katika kanisa la Roman Catholic Kigango cha Stalike Parokia ya Ilembo amewakabidhi wanakwaya wa kanisa hilo Kiasi cha Shilingi Laki Tano ili kufanikisha ununuzi wa kinanda hii inatokana na ziara aliyowahi kufanya kwenye kata ya stalike alipopokea taarifa ya maombi ya uhitaji wa ununuzi wa Kinanda.

Waumini wa kanisa hilo na wanakawaya wamemshukuru Mbunge huyo kwa moyo wa upendo kwa kuwasaidia kwaajili ya maendeleo kanisani hapo.

Mbunge huyo anatarajia kuanza Ziara katika jimbo lake la  Nsimbo kuanzia Tarehe 10/7/2023 kwenye kata zote za Jimbo la Nsimbo kwaajili ya kujionea kazi za maendeleo zinazotekelezwa kwenye Jimbo hilo na kuibua vipaji vya Wasanii wanyimbo za kizazi kipya na Ngoma za asili.

Katika ziara hiyo atapata fursa ya kukabidhi Pikipiki 12 kwa Makatibu Kata wa Chama cha Mapinduzi ngazi ya Kata zilizopo Jimbo la Nsimbo hii ikiwa ni ahadi aliyotoa wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ndani ya miaka Miwili katika Jimbo la Nsimbo.

kwa habari zaidi endelea kutembelea ukurasa wetu wa 

kataviclub.blogspot.com

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages