Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi,Bupe Mwakang"ata akizungumzia masuala ya DP-World ambapo amewapa elimu wananchi wa mkoa huo. |
Na Israel Mwaisaka,Nkasi.
MBUNGE wa viti maalumu mkoa wa Rukwa Bupe Mwakang'ata (CCM) amewaondoa hofu Wananchi juu ya uwekezeji bandarini unaofanywa na serikali na kuwapuuza wale wote wanaoukashifu uwekezaji huo kupitia DP WORLD.
Mbunge wa viti maalumu Bupe Mwakang'ata akikabidhi majiko ya gesi kwa Wanawake kama njia ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira. |
Amesema ni muda mrefu serikali imekua ikitafuta namna nzuri ya kuleta tija katika bandari zetu Nchini na moja ya njia hizo ni za uwekezaji na sasa wamejitokeza watu ambao wanaupinga bila sababu za msingi na kutaka waende wakawe mabalozi wazuri na kuelezea nia njema ya serikali juu ya uwekezaji ambapo sasa DP WORD wameonyesha nia ya kuwekeza katika eneo hilo la bandari.
"Uwekezaji katika eneo hili la bandari ni utekelezaji wa Ilani ya CCM
katika kukuza pato la taifa sasa wamejitokeza watu ambao ni wapotoshaji juu ya
uwekezaji huo wa bandari na sisi tukawe chachu ya kulisemea jambo hili na
kuuelimisha Umma juu ya umuhimu wa uwekezaji huo na tuwakemee wapotoshaji
hadharani" amesema Bupe.
Na amedai kuwa bandari ina changia sehemu kubwa ya pato la taifa hivyo eneo
hilo linahitaji maboresho ili tija zaidi ionekane na mojawapo ya kinachofanyika
ni uwekezaji na Watanzania watambue nia njema ya serikali katika uwekezaji huo.
Sambamba na hilo mbunge huyo katika kuunga mkono jitihada za Mama Samia Suluhu
Hassan za kukabiliana na uharibifu wa mazingira amewakabidhi Wanawake hao kila
mmoja jiko la kupikia la Gesi ili kupunguza matumizi ya kuni yanayopelekea
misitu kukatwa na kupata kuni.
Alisema kuwa njia sahihi ya kukabiliana na ukataji wa miti kiholela ni kuwa na
matumizi ya nishati mbadala ikiwemo gesi na kutaka majiko hayo yatumike
ipasavyo ili kuachana na matumizi ya kuni.
Mwenyekiti wa UWT wilaya Nkasi Beatrice Ngua kwa upande wake alimshukuru Mhe,Mbunge kwa kujitoa na kuwakabidhi mitungi hiyo ya gesi zaidi ya 70 na kuwa wao watayatumia vyema ikiwa ni pamoja na wao kwenda kuwa chachu kwa Wanawake wenzao juu ya matumizi ya nishati mbadala badala ya kutegemea kuni pekee ili kuweza kuyalinda mazingira.
Na alidai kuwa wao watajitahidi kuuelimisha Umma juu ya nia njema ya serikali ya kuboresha utendaji wa bandari Nchini na uwekezaji katika eneo hilo haukwepeki na kumtaka kila mmoja akawe mstari wa mbele kulisemea hilo ili jamii iweze kuelewa na kuwapinga wapotoshaji wote.