MB: MARTHA AWAKUMBUSHA WAZAZI MAPAMBANO UKATILI KWA WATOTO

Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Katavi Martha Mariki akizungumnza na wanawake wa jumuiya ya UWT kata ya Mwese na Kutuma kuhusu wajibu wa wazazi na walezi kuwalinda watoto wao dhidi ya ukatili wa kijinsia

Na Paul Mathias,Katavi

Wazazi na walezi Katika mkoa wa Katavi wameaswa kuwajibika ipasavyo katika malezi ya watoto wao Ili kukabiliana na tatizo la ukatili wa kijinsia Kwa watoto ambao umekuwa ukilipotiwa dhidi ya watoto kwenye mkoa wa Katavi.

Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Katavi,Martha Mariki akikabidhi shilingi Laki Tano na kadi 200 za chama cha Mapinduzi CCM kwa viongozi wa UWT kata ya Mwese.

Wazazi na walezi Katika mkoa wa Katavi wameaswa kuwajibika ipasavyo katika malezi ya watoto wao Ili kukabiliana na tatizo la ukatili wa kijinsia Kwa watoto ambao umekuwa ukilipotiwa dhidi ya watoto kwenye mkoa wa Katavi.

Wito huo umetolewa na Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki wakati akizungumnza na Wanawake wa umoja wa chma Cha mainduzi CCM katika kata za Mwese na Katuma katika wilaya ya Tanganyika akiwa ktika ziara ya kutembelea kata zote za mkoa wa katavi.

‘’tuna tatizo la Watoto wetu kufanyiwa vitendo vya ukatili wa Kijinsia ubakaji,na kulatiwa mama zangu niwaase tuzungumnze na watoto wetu tusiwaonee haya amesema Martha’’

Viongozi wa chama na serikali kata ya mwese wakimsikiliza Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa katavi Martha Mariki alipotembelea kata hiyo

Amesema baadhi ya sababu zinazo pelekea kutoa Kwa vitendo hivyo ni pamoja na baadhi ya jamii kuamini Imani za kishirikina katika kufanikisha baadhi ya masuala katika maisha yao.

‘’maendeleo yanakuja Kwa kufanya kazi hawawanaoamini ukimlawiti au kumbaka mtoto mdogo ili upate maendeleo hizo ni imani potofu tuendelee kuzipinga kwa kwenda kuwa mabalozi wazuri Kwa wenzetu huko tutokako''

Katika hatua nyingine ameishauri jamii pamoja na kwamba jamii inatumia muda mwigi katika shughuli za kiuchumi nivyema ikakumbuka malezi ya watoto hasa usalama wao pindi wazazi na walezi wakiwa katika shughuli za uzalishaji Mali.

Martha anasema‘’najua tutasema tupo katika shughuli za kiuchumi muda mwigi ni sawa ila tujenge mazoe ya kuzungumza na watoto wetu awe wa kike au wa kiume juu ya mwenendo wake wa siku nzima’'

Akiwa katika Ziara Kwenye Kata ya Mwese na Katuma Wilaya ya Tanganyika ametoa rai Kwa vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM na umoja wa wanake kujitokeza Kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa ili kutengeneza Msingi mzuri kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.

Mh Martha meipongeza serikali ya awamu ya Sita ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan namna inavyoendelea kuimalisha huduma za jamii katika sekta za Afya,Maji,Barabara, Kilimo na Elimu kupitia miradi mbalimbali ambayo inaendelea kutekelezwa katika mkoa wa Katavi.

Hadi Sasa Mbunge huyo wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki ametembelea  Kata kumi Karema,Ikola,Isengule,Kapalamsenga,Mnyagala,Kabungu, Kasekese ,Sibwesa, Mwese na Katuma .

katika Kata hizo ameweza kutoa shilingi Laki Tano Kwa Kila Kata Kwa lengo la kuwainua Wanawake wa UWT kujikwamua kiuchumi pamoja na kutoa kadi 2000 za UWT Kwa mkoa wa Katavi  na Kutoa Jalala 120 kwa UWT Mkoa wa Katavi.

Kata zilizobakia kuwatembelewa na Mh Martha Mariki ni kata za Mishamo,Bulamata,Ilangu, Ipwaga,Tongwe ,na Majalila huku ziara hiyo ikiwa inaendelea.

kwa habari zaidi endelea kutembelea ukurasa wetu wa 

kataviclub.blogspot.com

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages