Na Walter
Mguluchuma,Katavi.
Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wanahakikisha wanaendelea kusimamia kwa nguvu zote miradi ya maendeleo yote inayotekelezwa kwenye Manispaa ya Mpanda kwa ukaribu zaidi na kwa kuzingatia thamani ya fedha ili kutomwangusha Rais kwenye utekelezaji wa miradi ya Maendeleo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Sofia Kumbuli akiwaelezea madiwani wa Baraza la Madiwani namna ambavyo Manispaa hiyo ilivyopanga kutengeneza madawati 4000 kwa ajiri ya Shule za Msingi ili kuondokana na upungufu wa dawati katika shule za Msingi za Manispaa |
Kauli hiyo ya Manispaa ya Mpanda imetolewa na Meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry wakati aliipokuwa akifunga kikao cha robo ya nne cha Baraza la Madiwani la Manispaa hiyo kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa kilichojadili taarifa mbalimbali za utendaji kazi wa Kata za Manispaa ya Mpanda .
Alisema wanaendelea kusimamia miradi yote
inayotekelezwa kwa ukaribu zaidi ili kuhakikisha miradi hiyo
inatekelezwa kwa ubora na kiwango kinachotakiwa kulingana na thamani
ya pesa ambazo zinazokuwa zimetolewa kwa ajiri ya
utekeleza wa miradi husika .
Sumry ameeleza kuwa miradi yote ambayo wameitekeleza na
inayoendelea kwenye Manispaa ya Mpanda inaonekana jinsi
ilivyotekelezwa na ilivyosimamiwa kwa ufanisi mkubwa na
kwa kuzingatia ubora unao lingana na thamani ya fedha .
Amesisitiza kuwa hawako tayari
kumwangusha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye
utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwani katika kipindi
cha miaka miwili yapo mengi yamefanyika kwenye Manispaa hii
ya maendeleo .
Hivyo wataendelea kusimamia miradi yoye inayoletwa na Serikali ya awamu ya sita ili kuhakikisha wananchi waote wanapata huduma nzuri na bora kama ambavyo Rais Samia alivyokusudia.
Madiwani wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wakiwa kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wakipotea taarifa za utendaji kazi wa Kata mbalimbali |
Amesema kuhusu vituo vya afya vilivyojengwa hivi karibu
vituo vyote wameisha weka umeme isipo kuwa vituo viwili
tuu hata havyo Mkuu wa Mkoa wa Katavi
ameisha liagiza shirika la umeme Tanesco kuweza kufikisha umeme kwenye
vituo hivyo vya afya ifikapo tarehe 30 ya mwezi huu
.
Diwani wa Kata ya Mwamkulu Kalipi
Katani amesema kuwa miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye
Manispaa ya Mpanda imekuwa na ubora mkubwa na aliomba kwenye Kata yake
waongeze walimu wa kike kwenye shule ya Msingi Mkokwa ambayo inaupungufu
wa walimu wa kike.