WAZAZI WAONYWA KUTOKUWA CHANZO NDOA ZA UTOTONI.

Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi,Martha Mariki akiwa katika kikao na wanawake wa UWT Kata ya Kakese na wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM 

Na Paul Mathias,Katavi.

Serikali Katika Mkoa wa Katavi imesema haita sita kuchukua hatua Kali za kisheria Kwa baadhi ya wazazi na walezi ambao wamekuwa na tabia ya kuwaozesha watoto wao wa kike katika umri Mdogo badala ya kuwapeleka shule kupata Elimu.

Wanawake wa UWT Pamoja na wanachama wa chama cha Mapinduzi Kata ya Kakese wakimsiliza Mbunge wa viti maalumu Martha Mariki katika kikao hicho

Serikali Katika Mkoa wa Katavi imesema haita sita kuchukua hatua Kali za kisheria Kwa baadhi ya wazazi na walezi ambao wamekuwa na tabia ya kuwaozesha watoto wao wa kike katika umri Mdogo badala ya kuwapeleka shule kupata Elimu.

Akizungumnza na Wanachama wa chama Cha Mapinduzi (CCM)  na wanawake wa (UWT)  Katika Kata ya Kakese Manispaa ya Mpanda unMbunge wa Viti maaalum Mkoa wa Katavi,Martha Mariki amekemea vikali hali hiyo ya kuwaozesha watoto wa kike Kwa tamaa ya kujipatia Mali .

‘’unakuta mtoto amefaulu lakini mnafanya njama badala ya mtoto kwenda shule mnakwenda kumuozesha kwa tamaa ya Mali haikubaliki niwaambieni mkiwaozesha watoto ambao wanapaswa kuwa shule mtakuja kukosa viongozi na sisi hatutakubali hili liendelee’’

Amesema kuwa Kila mtoto anahaki ya kupata Elimu na siyo vyema kukatiza ndoto za watoto Kwa kuwaozesha hali ambayo hupelekea kukosa viongozi wa kesho kutokana na baadhi ya walezi kuozesha watoto wa kike.

‘’Msikubali kufanya vitendo vya kuwaozesha watoto wa kike kwa tamaa ya Ng’ombe ukiwa na binti yako aliesoma vizuri atakusaidia niwaambieni watoto wa kike wanauchungu sana wa wazazi kuliko hata watoto wa kiume mimi nimezaliwa katika familia ya watoto wakike watano lakini Baba hajawahi kukata tamaa ametusomesha na leo hii anaona Matunda tuache kuwaozesha watoto wa kike tuwapeleke shule’’

Nicolaus Lukene  mkazi wa Kijiji Cha kakese amesema kumekuwa na hali Kwa baadhi ya wazazi na walezi kuwaozesha watoto wao katika umri Mdogo badala ya kuwapeleka shule Kwa kuwa na tamaa ya kujipatia Mali kupitia mahali.

’Unakuta mtoto anaozeshwa akiwa na umri mdogo miaka kumi na tatu hadi kumi na nne lengo kuu mzazi apate Ng’ombe nane hadi kumi na kuemdelea hii inawanyimafursa watoto hawa kupata elimu’’

Kwa upande wake Helena Lucas Kapitao mkazi wa Kijiji Cha kakese amesema wazazi watafute Mali ya halali Kwa kufanya kazi na sio kutegemea Mali zinazotokana na kuwaozesha watoto badala ya kuwapeleka shule.

 ‘’Wazazi tutafute Mali Kwa kufanya kazi unakuta mzazi mtoto wake wakike amefaulu kwenda sekondari badala ya kumpeleka shule utasikia amemuozesha tuiombe serikali watu kama Hawa wasionewe haya’’.

Helena  ametoa ushauri Kwa wakazi wa Kakese kuacha tabia hiyo Kwani Huwa nyima watoto wao fursa ya kupata Elimu na hatimae kushidwa kufikia ndoto zao za Maisha inayotokana na Elimu 

Katika ziara hiyo Mbunge wa Viti maalumu katika mkoa wa Katavi Martha Mariki ametoa shilingi Laki Tano kwa kila kata ambazo amezitembelea Leo ambazoni Kata ya Kakese na Misunkumilo ili kuwasaidia wanawake wa UWT Kata hizo kujikwamua kiuchumi pamoja na kutoa kadi za UWT Kwenye Kata hizo Kwa lengo la kuendelea kuongeza wanachama wa UWT Kwenye kata zao.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages