MWENYEKI WA KIJIJI TANGANYIKA AKIMBIA MKUTANO WA WANANCHI.

 

Mwenyekiti wa Kijiji cha Lwega,Salumu Kibelenge akiwa katika Kijijji cha Kapanga alikokimbilia akikwepa kikao cha wananchi wa kitongoji cha Manyonyi Kijiji cha Lwega baada ya kufuatwa na wanahabari- Picha na George Mwigulu.

Na Paul Mathias,Tanganyika.

Wananchi katika Kitongoji cha Manyonyi Kijiji cha Lwega Kata ya Mwese halmashauri Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi wameiomba serikali kuingilia kati Mgogoro wa Aridhi ulipo baina yao na Serikali ya Kijiji.

Moja ya Mwananchi akionyesha Barua ya Wito kwa Viongozi wa Kijiji cha Lwega kuhudhuria Mkutano huo kwenye Kitongoji chao cha Manyonyi[ Picha na George Mwigulu]
Wananchi hao katika kuhakikisha suala hilo linatatuliwa wameamua kufanya kikao cha kujadili tatizo hilo kwenye Kitongoji chao licha ya uongozi wa Kijiji kutohudhuria kikao hicho baada ya kujulishwa kwa maandishi juu ya uwepo wa Mkutano huo.

Josephati Magoli mkazi wa Kitongoji hicho amesema kuwa maeneo maeneo hayo wamekuwa wakiishi kwa muda mrefu na wanashangazwa na uongozi wa serikali ya kijiji ya kuwataka kuondoka kwenye maeneo hayo kwa kile kinachodaiwa eneo hilo limetegwa kwa ajili ya malisho.

Josephati anasema ‘’mimi najua nimedhurumiwa haki yangu kama mtanzania na kesho watapokuja watasema wewe hujapimiwa ni Mkimbizi ondoka nitaenda wapi mimi na watoto wangu Mh Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na waziri Mkuu Kassimu Majaliwa na waziri wa aridhi Anjelina mabula watusikie watanzania wa kitongoji chetu cha Manyonyi watusaidie ‘’

Kwa upande wake Mahembo Jilala amesema kuwa wamekuwa wakitakiwa kuondoka kwenye maeneo yao wanayoishi kwa kupisha maeneo hayo kuwa maeneo ya malisho hali ambayo inawafanya kuishi kwa wasiwasi.

‘’yaani tatizo kubwa lililotokea hapa Mashamba yetu tumenyanga’nywa na ofisi ya kijiji inadai kwamba yale ni malisho ya Ngo’mbe ambapo sisi tumeambiwa tufukuzwe kabisa tuondoke bila ya kujua tutaenda wapi "amesema Jilala.

Ameeleza kuwa madai hayo ya maeneo yao kuwa sehemu ya malisho wao hawakushirikishwa  hawakushirikishwa na wanashangzwa na hatua hiyo ya kuondolewa kwenye maeneo yao.

Zainabu Nyerere Mkazi wa Kitongoji hicho ameiomba serikali kuwarudishia maeneo yao ambayo wamekuwa wakiishi kwa muda mlefu na kuyafanyia shuhguli za uzalishaji mali ikiwemo kilimo na ufugaji.

’mimi naomba kikubwa tunaomba eneo letu wanatunyanga’nya tunamiaka mingi hapa wanatuambia kwamba ni maeneo ya malisho na kututaarifu hakuna tuende wapi tunawatoto tunaomba eneo letu’’

Mwenyekiti wa Kijiji cha Lwega Benedctor Salumu Kibelenge amesema kuwa Mwaka 2014 kulifanyika mpango wa matumizi bora ya Aridhi ambayo yalielekeza kutenga maeneo ya Kilimo,Makazi,Mistu na  Malisho

Amesema Mwaka 2020 kulifanyika Mapitio ya Mpango wa Matumizi bora ya Aridhi wa Mwaka 2014 ambapo wananchi katika mkutano huo 2020 walilalamika kuwa eneo la Malisho lililotengwa ni kubwa sana .

Kibelenge anasema ‘’baada ya kutenga maeneo hayo ilionekana eneo la Malisho wananchi wakalalamika kwamba eneo la malisho limekuwa kubwa inatakiwa lipunguzwe ili tupate eneo la kulima kwa hiyo tulifanya mapitio 2020 kulejea ule mpango ili wakulima kutokana na jinsi walivyozungumnza kwenye mkutano ili waweze kupata maeneo ya kilimo’’

Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo wa kijiji amesema kuwa katika mpango huo wa mwaka 2020 maafisa walipima maeneo ya kilimo na makazi nasio malisho ambayo wananchi wanalalamikia.

‘’maeneo walikuja kupima wale watalaamu ni maeneo ya Kilimo na Makazi tu si maeneo ya Mistu na maeneo ya Malisho hivyo kama kuna maafisa aridhi ambao walipima basi walipima kimakosa sababu eneo la malisho halipipwi na kama kuna watu walipimiwa kwa utaratibu huo basi ilikuwa kinyume na utaratibu kimsingi eneo lote la malisho halikutakiwa kupimwa na hivi hata kama ukimpigia kiongozi aliehusika na upimaji atakuambia walipima maeneo ya makazi na kilimo tu ‘’amesema Mwenyekiti huyo wa Kijiji cha Lwega

Kiberenge ameeleza kuwa mchakato huo wa mapitio ulishirikisha wananchi kupitia mkutano wa hadahara pamoja na viongozi wa Kijiji na Kitongoji hicho kufanyika kwa mapitio hayo ya kupunguza eneo la malisho kubakia kuwa eneo la kilimo.

‘’kwenye mkutano huo tuliwashirikisha wananchi wa Kitongoji cha Manyonyi walitoa wawakilishi ambao tulikuwa tunazunguka nao pia tulikuwa na uongozi wote wa Kijiji na tulizungnza kwamba eneo la malisho kupunguzwa liwekwe sehemu fulani hivyo tuliwashirikisha’’Amesema Kibelenge.

Kuhusu taarifa ya mwaliko wa mkutano huo kufanyika kwenye kitongoji hicho amesema alipata taarifa ya Maandishi kuhitajika kwenye mkutano huo kupitia mwenyekiti wa Kitongoji lakini kutokana na majukumu mengine ya kiserikali hakuhudhuria mkutano huo baada ya kuhitajika mkoani kwa majukumu ya kiserikali.

Amesema Mwananchi huyo‘’mimi nilipata udhru nikaenda Mpanda mjini kwa mambo ya kiserikali baada ya hapo nilipigiwa simu na mwenyekiti wa kitongoji kuwa kuna barua yako ya wito wa mkutano unahitajika kwaajili ya mkutano na wananchi’’

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages