MBUGE MARTHA ATOWA MIL MOJA UJENZI WA KITUO CHA AFYA.


Mbunge wa Viti maalumu wa Mkoa wa Katavi,Martha Mariki akipiga ngoma ya asili ya kabila la Wahutu  na wakazi wa kijiji cha Ilangu Wilaya ya Tanganyika wakati wa ziara yake ya kikazi.


Na Paul Mathias,Tanganyika.

Mbunge wa Viti maalimu Mkoa wa Katavi, Martha Mariki ametoa shilingi Milioni Moja Kwa wananchi wa Kata ya Ilangu kama sehemu ya kuwaunga mkono katika jenzi wa kituo Cha Afya.

Martha Mariki,Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Katavi akiwahutubia  leo wananchi wa kijiji cha Ipwanga wilaya ya Tanganyika.

Mbunge wa Viti maalimu Mkoa wa Katavi, Martha Mariki ametoa shilingi Milioni Moja Kwa wananchi wa Kata ya Ilangu kama sehemu ya kuwaunga mkono katika jenzi wa kituo Cha Afya.

Akizungumnza na wananchi hao katika mkutano wa Hadhara uliofanyika  Kijijini Ilangu ikiwa ni sehemu ya ziara ya Mbunge huyo kutenbelea Kata za Mkoa wa Katavi.

Martha amesema kuwa ameguswa na kujitoleo kwa wananchi wa Kata hiyo Kwa kufyatua tofali za kutosha kwaajili ya ujenzi wa kituo hicho Ili wananchi wapate matibabu pindi Kituo hicho kitakapo kamilika.

Martha Mariki,Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Katavi akiwahutubia leo wananchi wa Kata ya Ilangu wilaya ya Tanganyika ambapo aliweza kutoa kiasi cha Tsh 1,000,000/- kama juhudi za kuunga mkono ujenzi wa kituo cha afya.

'nimesikia kupitia taarifa ya viongozi wenu kuhusu mchakato wa ujenzi wa Kituo Cha afya mmefatyua tofali za kutosha Sasa Mimi kama Mbunge wa Viti maalumu nawachingia shilingi Milioni Moja keshi Ili feddha hii isapoti ujenzi huu'' amesema Martha

Amebainisha serikali imeendelea kuboresha huduma za afya kwa ujenzi wa vituo vya afya na hospital katika wilaya ya Tanganyika Mkoa wa katavi na  kuwapongeza wananchi hao kwa kuunga mkono juhudi za serikali Kupitia kujitolea ya nguvu kazi.

Diwani wa Kata ya Ilangu,Agustino Sadiki Mathew amemshuru mbunge  Martha Mariki na kuahidi fedha hizo kuzisimamia zifanye kazi iliyo kusudiwa kwa kishirikina na viongozi wenzake.

Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Katavi,Martha Mariki akikabidhi kiasi cha fedha kwa viongozi wa kata ya Bulamata wilaya ya Tanganyika wakati wa ziara yake ya kikazi,

Moja ya kiongozi wa Kata ya Bulamata akionesha fedha kwa wananchi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika leo katani hapo,ambapo fedha hizo zimetolewa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Katavi,Martha Mariki.

Mbunge huyo yupo katika ziara ya kutembelea Kata za Mkoa wa Katavi ambapo ametembelea Kata za Ilangu na Ipwaga na kutoa Tsh 500,000/-  kwa kila Kata ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake ya fedha Mil 29 kutoa kwa UWT Kwa leongo la kuwainua Kiuchumi wanawake.

Pamoja na hayo Mbunge huyo ameweza kutoa kadi 2000 za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa wanawake wa UWT Mkoa wa Katavi.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages