MBUNGE LUPEMBE APANIA KUWA NA TIMU INAYOSHIRIKI LIGI YA NBC.


Mbunge wa Jimbo la Nsimbo,Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Anna Lupembe akitoa fedha ya Tsh 500,000/- kwa timu ya Kata ya Tumaini  baada ya kuibuka mshindi kwenye mashindano hayo.

Na George Mwigulu,Nsimbo.

Wachezaji arobaini wa mpira wa miguu katika Jimbo la Nsimbo wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi watachaguliwa wakati wa ligi ya jimbo (LUPEMBE CUP) kwa ajili ya kuingia kambi ya kuendeleza vipaji na kutengeza timu itakayowezesha mbio za kushiriki ligi kuu Tanzania bara (NBC).

Mbunge wa Jimbo la Nsimbo,Anna Lupembe (Kulia) akizungumza leo na wananchi wa Kijiji cha Tumaini wakati ya hafla ya kukabishi zawadi kwa washindi wa mpira wa miguu wa kata ya Itenka na Tumaini.

Kwa miaka mingi mkoa wa Katavi licha ya juhudi mbalimbali kufanywa na viongozi na wadau wa michezo lakini umekosa timu hata moja inayoshikiri kwenye mashindano mbalimbali hususani NBC.

Akizungumza kwenye mkutano leo katika kijiji cha Tumaini Kata ya Itenka halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoani hapa,Mbunge wa Jimbo la Nsimbo,Anna Lupembe ameeleza kuwa lengo kubwa kwenye mashindano ambayo amekuwa akiyafadhili ni kuibua vipaji kwa vijana hasa kupitia michezo kama inavyoelekezwa kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Lupembe ameeleza kwa muda mrefu amekuwa akifadhili mchezo wa mpira wa miguu katika jimbo lake kupitia ligi ya Lupembe CUP ambapo amebaini kuna vijana wengi wanavipaji vikubwa hivyo hawezi kuviacha pekee kwenye hatua ya chini na kupotea.

Mbunge huyo amefafanua kwa sasa mashindano ya kutafuta washidi kila kata za kimchenzo 16 alizozianzisha kutokana na ukubwa wa kijiografia wa jimbo hilo yamekamilika na jumla ya fedha Tshs 30,880,000/= zitatumika.

Ameeleza kuwa tayari ugawaji wa zawadi wa fedha hizo ameanza kutoa kwa kila kata ya Itenka na Tumaini ambapo mshindi wa kwanza amepewa Tsh 500,000/=,wa pili Tsh 300,000/= wa tatu Tsh 200,000/= wa nne Tsh 100,000/= nawa tano Tsh 50,000/= kama kifuta jasho.

“…hatua ambayo nitaichukua baada ya kuanza ligi ya Lupembe Cup ambayo baada ya kupatikana washindi ngazi ya kata za kimichenzo 16 kutakuwepo na wataalamu wa soccer ambao watachangua wachezaji 40 wenye vipaji ambapo wataingia kambi kwa ajili ya kujifua ili kuanza mikakati ya kuanza kushiriki ligi ngazi mbalimbali hadi kufikia ligi daraja la tatu.Lengo kubwa ikiwa ni kushiriki ligi kuu” Amesema Mbunge Lupembe.

Hata hivyo Mbunge huyo amesema licha ya ligi ya Lupembe Cup itaibua wachezaji 40 watakao chaguliwa kwenda kambi maalumu bali ameahidi kiwango cha juu cha utoaji wa zawadi ambapo mshindi wa kwanza atapatiwa ni Tsh Milioni moja huku akisema “nimeona hata hivyo manufaa makubwa kwa sababu vijana wengi wameweza kufuatwa na timu mbalimbali na kujiunga nazo”.

Aidha katika kutambua umuhimu wa kuwa na wataalamu wa masuala ya soccer jimbo la Nsimbo amesema Lupembe tayari ameweza kulipa fedha zaidi ya Mil 3 kuwapeleka watu kwenye mafunzo ya kupata waamuzi bora wenye uwezo wa kuchangua sheria 17 za soccer ambapo wameweza kuhitimu na kutunukiwa cheti.

 Wile Masanja mmoja ya wadau wa mpira wa miguu katika kata ya Itenka licha ya kumshukuru mbunge huo pia amewaomba vijana kuchangamkia fursa hiyo kujitokeza zaidi na kuonesha uwezo wa kucheza mpira.

Mdau huyo ameeleza kuwa michezo kwa dunia ya sasa ni ajira kubwa ambayo imewatajirisha wachezaji na kuchangia mapato mataifa yao ya kiuchumi.

Rashidi Juma,Mchezaji wa Mpira wa miguu na Makazi wa Kijiji cha Tumaini amesema kuwa jambo ambalo analifanya mbunge nila kukubwa daima kwenye mioyo yao kwani kwa muda mrefu walikosa ni nani ambaye anaweza kuwafadhili.

Asema utoaji wa zawadi ya fedha ni motisha kubwa kwao inayowafanya kujituma zaidi kwenye kucheza mpira ambapo wanaimani hawataweza kumwangusha pale ambapo wataanza kushiriki kwenye michuano mikubwa kuelekea kuwa na timu inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara (NBC).

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages