MBUNGE HEKARI 13.844 KUTOKA ENEO LA HIFADHI WAMEPEWA WANANCHI NSIMBO

Mbunge wa Jiimbo la Nsimbo,Anna Lupembe akizungumza na wananchi katika kitongoji cha Mgolokani kijiji cha Matandalani leo wakati wa ziara yake ya kikazi jimboni hapa.

Na George Mwigulu, Nsimbo.

Serikali imetoa ardhi ya jumla ya hekari 13,844 kwa wananchi wa kata ya Sitalike halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi kutoka kwenye maeneo ambayo yalikuwa chini ya hifadhi ya taifa ya wanyamapori (KANAPA) kwa ajili ya kuendeleza shughuri za binadamu.

Baadhi ya wananchi wa kata ya Sitalike wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika kitongoji cha Mgolokani kijiji cha Matandalani leo ambapo wamemsikliza Mbunge wa Jimbo la Nsimbo,Anna Lupembe akiwahutubia.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mbunge wa Jimbo la Nsimbo,Anna Lupembe wakati ajibu swari la Mzee Leonard Kazimoto,Mkazi wa kitongoji cha Mgolokani kijiji cha Matandalani ambapo amehoji ni lini serikali itaacha tabia ya kumega ardhi kutoka kwa wanadamu na kuwaongezea wanyamapori ili hali watu wanazidi kuzaliana na kuongezeka.

Mzee huyo pia amehoji kuwa haoni juhudi zozote zikifanywa na viongozi wa serikali kutekeleza ahadi ya aliyekuwa rais wa awamu ya tano Hayati Dkt John Magufuli ya kugawiwa ardhi ambayo ni sehemu tu ya hifadhi hiyo ambayo aliitoa wakati wa ziara yake mkoani Katavi.

Mbunge huyo wakati akijibu amesema kuwa serikali tayari imeshatoa ardhi kwa wananchi wa maeneo hayo ambapo zaidi ya hekari 5092 ni kwa ajili ya wakulima pamoja na hekari 7752 kwa ajili ya wafugaji.

Lupembe ameeleza kuwa serikali inatambua umuhimu wa wananchi kuwa na ardhi ya kutosha kwa ajili ya kuendesha shughuri za kilimo na ufugaji ili waweze kujikwamua kwenye mdororo wa kiuchumi hivyo ikotayari kukikisha watu wanakuza mapato yao na taifa kwa ujumla kupitia kilimo na ufugaji.

Vilevile amtoa rai kwa kusema “kunawengi wanajiwekeza hekari 300 hadi 400 na sisi katika eneo letu hili ni eneo ambalo liko nisema kwa kiingereza “sensitive”(Nyeti) sana kwa sababu tunawanyama tukibeba heka zote hizo peke yako ukawanyima haki wenzio basi tugawane kidogokidogo ili kila mmoja apate pakulima ”.

"unaweza kuchukua hekari zote hizo matokeo yake ukaziacha usizifanyie kazi ukawa unazitizama tu mwenzako anakufa na njaa hivyo haipendezi sana" Amesisitiza Mbunge huyo.

Hata hivyo Lupembe amesema anatabua ziko bado changamoto kwenye maeneo hayo ya watu wanaoishi kuzunguka hifadhi ya KANAPA ambapo ameahidi kuongea na viongozi wa hifadhi hiyo kwa ajili ya kuwakutanisha na kutafuta ufumbuzi.

Baadhi ya wananchi wakiwa wamepata mtini wakati wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Nsimbo,Anna Lupembe leo katika kitongoji cha Mgolokani Kijiji cha Matandalani.

“ nafahamu tuna mto wetu wa sitalike na tulikuwa na wavuvi ambao walikuwa wakivua samaki kupitia huo,mimi kama mbunge wenu nimeenda kuongea na Kamishina Mkuu wa TANAPA aje tukae sisi wananchi na pamoja yeye tukubaliane na kupata mwafaka kwa sababu tulikuwa tukipata kipata pale” amesema Lupembe.

Nao baadhi ya wananchi,Hawa Rammadhani wamemshukuru mbunge huyo kwa kazi nzuri anayoifanya hususani kwa kuwapigania kupata ardhi hiyo kwani walikuwa wamekosa matumaini.

Hawa amesema wanaimani kuwa kupitia utaratibu utakao wekwa wataweza kugawiwa vema na kuendeleza shughuri zao za kilimo na ufugani.





Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages