WANANCHI WA MSHUKURU RAIS SAMIA KWA HUDUMA YA MAJI

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki akimtua ndoo kichwani Mkazi wa Kjiji cha Mwamkulu alipotembelea Mradi wa Maji ambao unawanufaisha Wananchi kwa kujipatia Maji Safi na Salama.

 
Na Paul Mathias,Mpanda

Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki ameishukuru serikali kwa kuwaletea Huduma ya Maji safi na Salama wa kazi wa Kata ya Mwamkulu Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.


Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki ameishukuru serikali kwa kuwaletea Huduma ya Maji safi na Salama wa kazi wa Kata ya Mwamkulu Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.

Akiwa katika ziara ya kutembelea Kata zote za Mkoa wa Katavi amefika na kujionea namna mradi huo unavyo wasaidia wananchi kupata huduma ya Maji kwa uhakika tofauti na hapo siku za nyuma ambapo wananchi walikuwa wanatumia Maji ambayo si safi na salama.

‘’tunaishukuru sana serikali ya awamu ya Sita ya Mama yetu Dk Samia Suluhu Hassan kwa jinsi alivyo dhamilia kumtua mama ndoo kichwani’’

Amesema kuwa kazi ya serikali nikuhakikisha inawaletea wananchi wake Maendeleo yanayo onekana kwa macho hivyo upatikanaji wa huduma hiyo ya maji ni sehemu ya serikali kutekeleza wajibu wake kwa msukumo wa uwakilishi wa wabunge bungeni kusemea changamoto husika na serikali kutekeleza kwa vitendo.

’Sisi kama wananchi wa Mkoa wa Katavi mimi kama mwakilishi wa kundi la wanawake na mwakilishi wa wananchi wa mkoa wa Katavi nasema naishukuru sana serikali yetu kutuletea mradi huu wa Maji wenye thamani ya Milioni 400.73 tunasema asante sana mama wananchi wa Mwamkulu wanasema asante kwa mradi huu’’.

Katika hatua nyingine ameipongeza Ruwasa kwa Mkoa wa Katavi kwa usimamizi makini ambao umewezesha wanachi hao kupata huduma ya maji safi na salama kwa wakati pasipo na ucheleweshaji wa aina yeyote.

‘’nashukuru Ruwasa Mkoa wa Katavi kwa namna ambavyo wameweza kusimamia mradi huu kuhakikisha mradi huu umetekelezeka kwa wakati na wananchi wa Mwamkulu wameweza kupata maji’’

Katika ziara hiyo Mbunge Huyo amepata fursa ya kuzungumnza na wanawake wa UWT Kata ya Mwamkulu na kuwapatia kiasi cha shilingi Laki Tano ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Magreth Robert Mkazi wa Kijiji cha Mwamkulu amesema huduma hiyo ya upatikanaji wa maji imewaepushia kutumia muda mwingi kutafuta Maji kitendo ambacho kilikuwa kinaathiri shuhguli za uzalishaji mali kijijini hapo.

‘’namshukuru Rais Samia wa awamu ya Sita ametusaidia sana kutuletea Maji kwa sasa tunashukuru kwa sasa kuna unafuu tunamshuru Mama Samia popote pale alipo’’

Kalipi Katani Diwani wa Kata ya Mwamkulu amewashukuru wabunge wa mkoa wa Katavi kwa kuisemea kata ya Mwamkulu kwenye chombo cha uwakilishi wa wananchi Bungeni na hatimae kupata mradi huo wa Maji.

‘’tunawashukuru sana Wabunge wetu kwa kusimama kwa kauli moja kwa kuisemea Kata yetu sisi tunafarijika sana tunaendelea kuwaombea muwesalama pamoja na mama yetu Rais Wetu Dk Samia Suluhu Hassan’’

Amebainisha kuwa kabla ya Ujio wa Mradi huo wa Maji kwenye Kata yake walikuiwa wanalazimika kuchangia kutumia Maji na Wanyama hususani Ngo’mbe kwenye mito na Visimani.

Mradi huo utakwenda kunufaisha Mitaa mitatu  kwenye Kata hiyo  ambayo ni St Maria,Mkwajuni na Mkokwa ambayo ni sawa na Jumla wote ya wakazi 16,735 wa Kata ya mwamkulu wananufaika na Mradi huo wa Maji.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages